AFRICA: OCAMPO A PAINFUL THORN IN AFRICA

BON VOYAGE washukiwa wote wa vurugu za 2008 mkavune kile mlichopanda kwa kiburi na damu ya wanyonge. Sasa kumekucha Kenya. Haki na hujuma kuchuana. Raila na Kibaki kuchuana kuhusu viongozi hao waandamizi kukamatwa na kufikishwa ICC.

Kuna kila dalili kuwa Kibaki km mteuzi wa watuhumiwa kwenye serikali yake huenda asitoe kibali kirahisi kwa hao waandamizi wakamatwe na ndiyo maana wakati rais El Bashir alipokuwa Kenya serikali ya Kibaki haikumkamata kwa sababu ilijuwafika kuwa na wao kiyama chao kinakuja [same applies to Museveni], hivyo hii ni dalili tosha kbs kuwa Kibaki hataridhia watuhumiwa hao kukamatwa na kupelekwa The Hague na hapa ndipo waziri mkuu Raila atakapoanza kupiga jaramba ya kutaka haki itendeke na maamuzi halali ya ICC yaheshimiwe kwa kutekelezwa ndani ya Kenya iliyotia sahihi kuwa mwanachama wa ICC na hapa ndipo natabiri mwanzo wa mwisho wa Raila na Kibaki kuwa kitu kimoja.

Kibaki alisaidiwa na mauaji haya kuingia ikulu na hata Raila na wote wadadisi wa mambo wanajuwa hili waziwazi, ndiyo maana Kibaki hakuwa tayari kesi hii iendeshwe nje ya Kenya kwa sababu hata yeye inawezakumfanya El Bashir wa Kenya.

Kwa upande wa Raila, yeye ana utayari wa kujitokeza mbele ya haki kama angetajwa pia kwa sababu ni mzoefu wa siasa za misukosuko ya kudai haki ya umma na yuko tayari hata kuhitilafiana na rais lijapo swala la haki kwa umma na ndiyo maana hakusita kuridhia Ruto kuachia ngazi kwenye nafasi ya uwaziri wa elimu hata pale ambapo Kibaki alipomtetea Ruto kuwa aendelee kuwepo kazini km kawaida, ndipo Raila kwa uzoefu na umahiri wake wa kisiasa akamfungulia Kibaki darasa kuwa yeye Raila hakumfukuza Ruto kama anavyodai Kibaki kuwa yeye ndiyo ana uwezo wa kikatiba kumsimamisha kazi waziri ndipo Raila akam-elimisha Kibaki kuwa, ili haki itendeke inabidi Ruto awe pembeni ili apishe uchunguzi huru wa kashfa ya fedha ktk wizara yake, lkn pia Raila ndiyo mkuu wa upainzani ktk serikali ya umoja hivyo ni bosi wa Ruto, lkn pia ktk kuteuwa mawaziri makubaliano ni kuwa lzm rais akubaliane na upande wa pili wa serikali ya umoja wa kitaifa hapa ndipo Kibaki akaonekana kuwa hajui kutafsiri kanuni ambazo ndiyo nguzo za serikali ya umoja wa kitaifa.

Raila ni waziri mkuu mwenye nguvu na mvuto kuliko bosi wake, hali hii ndiyo inatatiza itifaki ya Kenya kila mara lijapo swala lenye kuhitaji uamuzi wa ngazi ya juu ya serikali. Nijuavyo Kenya, huu uamuzi wa ICC tayari ni mtaji mkubwa sana wa kisiasa kuelekea 2012 na kuwa hiki pekee ndicho kilikuwa kikwazo kilichobaki kwa Raila kutamalaki nchi ya Kenya 2012 hasa baada ya kupigana mpaka kupata katiba ambayo ni kitanzi kwa wasiopenda haki lkn mkombozi wa mnyonge, katiba ambayo imetafsiriwa kuwa hakuna Afrika nzima na lbd hata baadhi ya nchi za Ulaya ya kutolea mfano wake, hii yote ni jasho la Raila.

Niijuavyo Kenya ni kuwa tayari Kenya imeanza kampeni za 2012. Yaani tayari Raila ameishawapa katiba ambayo haikuwahi kuwepo na huenda isiwepo Afrika km siyo Kenya, pili kuzuia mishahara dhalimu ya wabunge ili kipaumbele kiwe ni maslahi ya walipa kodi, tatu swala la ICC pia ni mafanikio ya Raila, nne Raila lzm atapata support ya kimataifa endapo Kibaki hatapendezewa na speed yake kwa sbb kwa kitendo hiki cha ICC ni kuwa vinara wote wa ukabila wametokomezwa na km wamebaki basi ni wale wasio na nguvu na hivyo njia ni waaaaaaazi kwa Raila 2012, na hii ndiyo inayomnyima Kibaki usingizi kwa sababu lzm ya akina Kariuki, Ouko, Arwings Kodheks nk nayo yakawezekana ikiwa mpenzi wa wakenya ataingia ikulu 2012, lengo ni kuwa na political master plan au tuseme strategic plan ya kuiponya Kenya kabisa na makovu ya kihistoria [damu yoyote iliyomwagwa lzm siku moja itaibuka na kuongea tu].

Lkn pia Raila ana kikwazo kimoja tu cha umri kuelekea 2012 na ndiyo maana anajitahidi ili kuwa km atashindwa mpango wake wa kutaka kupigiwa mizinga 21 akiwa hai basi angalao ataingia kwenye historia ya Kenya ambayo hakuna mwanasiasa wa kizazi hiki ama kizazi cha babake ameweza ku-define Kenya mpya isipokuwa yeye mwenyewe AMOLO TINGA RAILA OGINGA ODINGA EARTHQUAKE.

Babake hayati AJUMA JARAMOGI OGINGA ODINGA [a star mathematician]alileta uhuru. Yeye RAILA AMOLO TINGA WICH KIDHER [ a mechanical engineer] ameleta Kenya mpya ambayo iliporwa na kufanywa mali binafsi ya mafisadi wa kisiasa na kiuchumi.

Lkn Raila ni mtu wa ajabu sana asiyetabirika kirahisi na hii tabia yake ndiyo inawapa wanasiasa wa Kenya homa za vipindi zisizopona kwa dawa yoyote, namaanisha kuwa hata Kibaki akiamua leo kumfukuza kazi [ingawa ni ngumu kwa sabau inawezazusha yale yale ya 2008 tena] yeye Raila haoni shida yoyote kwa sababu kwake hoja siyo cheo ila hoja ni kuona Kenya yenye maziwa na asali siyo tu inawezekana bali inapatikana pia kabla yeye Raila hajenda kaburini. Kibaki anatangaza kuimarisha ulinzi nchi nzima huku ICC nayo ikifanya jitihada za kuwahamishia nje ya Kenya mashahidi kwa kuhofu usalama wao, je, swali ni kwamba mbona Kibaki hakuimarisha ulinzi huo wakati ule wa vurugu zile za 2008 na badala yake leo dunia inashuhudia bosi wa polisi ambaye ni mteule wa Kibaki anasubiriwa kwa hamu kubwa kule The Hague.

Ocampo kiboko ya madhalimu wa Afrika akimalizana na Kenya na El Bashir huenda akabisha hodi Zim kukwaana na kisiki kilichomshinda UK na USA. Kweli Afrika ni kichaka cha majambazi.

BON VOYAGE washukiwa wote wa vurugu za 2008 mkavune kile mlichopanda kwa kiburi na damu za wanyonge. Tusalimieni Jean Bemba na Charles Taylor, muwaambie Afrika sasa haikaliki, mzungu amechachamaa na ICC yake, tena muwaeleze wamwaandalie nafasi bosi wa Zim km Tchangirai naye atacheza kete km za Raila na Kabila lkn wasichukue nafasi ya Hon. El Bashir ambaye huenda vikosi vya ujasusi vya Israel vikapata tenda ya kumkamata nyumbani kwake km walivyomkamata Savimbi na kumpumzisha jumla baada ya majeshi makubwa ya mataifa makubwa kushindwa.

Douglas Majwala.

One thought on “AFRICA: OCAMPO A PAINFUL THORN IN AFRICA

  1. Douglas O. Majwala

    Lkn pia wasiwasi ni kuwa Raila atapona kweli mbele ya Ruto? Kuna hatari kubwa kuwa Ruto akaamua kufa na Raila kwa kumtaja kuwa ni mhusika pia ukizingatia kuwa tayari hawaelewani, vivyo hivyo kwa Kibaki na Muthaura/Uhuru.

    Naona kama Ocampo anasubiri baada ya 2012 ili awasombe Raila na Kibaki pia, na kwamba kwa sasa wameachwa kwa sababu ya amani ya Kenya isichafuke tena km wakitajwa leo.

    Hali hii ndiyo inayofanya viongozi sasa waanze kampeni kali sana kwa ajili ya 2012 km kigezo cha kuwa wakifanikiwa kushika madaraka ya nchi 2012 huenda ikawa ngumu kutiwa matatani na Ocampo km ilivyo kwa El Bashir. Hii pia inawahusu washukiwa waliokwishatajwa na ICC, labda ICC ile njama na serikali kuwa washukiwa wote wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote Kenya ingawa hiyo pia ni kuwanyima haki yao ya kiraia/kikatiba kwa sababu bado ni watuhumiwa [siyo wahalifu]

    Amani ya Kenya huenda ikaingia dosari tena kabla ya 2012 km tahadhari haitazingatiwa kwa kiwango cha juu. Yale yale ya akina Ouko na Kariuki huenda yakatokea tena ili kufuta uwezekano wa baadhi ya watuhumiwa kufa na wenzao ambao hawajatajwa na ICC.

    Douglas Majwala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *