TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI itazipa wilaya za Tarime na Rorya mkoani Mara hadhi ya mkoa wa kipolisi kuimarisha ulinzi na usalama kukabiliana na wimbi la mauaji ya mara kwa mara katika maeneo hayo.
Akitangaza uamuzi huo mkoani Mara leo (Jumatano Julai 1, 2009) Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda alisema itaazishwa piakambi ya Jeshi la Kujenga Taifa na kuimarisha miundombinu ya barabara kwa madhumuni hayo hayo.
Waziri Mkuu alikuwa akihutubia sherehe za Siku ya Serikali za Mitaa kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma leo na baadaye alipotembelea maeneo yaliyokumbwa na mauaji katika wilaya za Rorya na Tarime leo (Jumatano, Julai 1, 2009).
Waziri Mkuu pia alisema anatoa miezi sita kwa uongozi wa wilaya hizo na mkoa kwa jumla kuandaa mkakakati na kuuwasilisha serikalini jinsi ya kukomesha mauaji hayo ama sivyo maeneo hayo yatatawaliwa kijeshi kwa kuwa utawala wa kiraia utakuwa umeshindwa.
“Madhumuni ni kuhakikisha amani na usalama wa raia katika maeneo hayo. Serikali imechoshwa na mauaji haya,” alisema.
Katika matukio ya hivi karibuni, zaidi ya wiki moja iliyopita, mpaka sasa watu 32 wameuawa katika mapigno kufuatia wizi wa ng’ombe watano ambao kati yao ng,ombe watatu walipatikana. Nyumba zaidi ya 400 zimechomwa na watu zaidi ya 3,000 wamekosa mahali pa kukaa.
Serikali imekwishadhibiti ulinzi na usalama katika maeneo hayo kwa kuowangeza nguvu za polisi na imeanza kutoa msaada kwa walioathirika.
Waziri Mkuu alisema ni aibu mauaji kama hayo kutokea nchini kwa hivi sasa lakini inaonekana pia kuwa viongozi wa wa kiraia wa maeneo hayo wameshindwa kazi kwani ni wajibu wao kuyazuia tangu mapema.
Alisema Serikali inachukua hatua za hadhari hivi sasa za muda mfupi, lakini za muda mrefu zitategemea mkakati wa viongozi wa wilaya hizo za Tarime na Rorya na mkoa mzima wa Mara.
Waziri Mkuu pia alitembelea kwa helikopta na kutuaalipata kwenye maeneo yaliyotokea maafa hayo katika wilaya za Rorya na Tarime na kuzungumza na wananchi. Aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali SaidMwema ambaye amekuwepo mkoani Mara kwa siku kadhaa akiwa na baadhi ya makamanda wake wakuu.
Katika eneo la Changuge, wilayani Rorya, wananchi waliopewa nafasi na Waziri Mkuu kutoa kero zao walimthibitishia kuwa mauaji hayo siyo ya kikabila na ya koo kati ya Wakurya wa Tarime na Wajaluo wa Rorya bali ni kati ya raia wema na majambazi wezi wa mifugo.
Waliiomba Serikali kuimarisha ulinzi kwa kuongeza askari polisi na zana.
Mbunge wa Rorya, Prof. Philemon Sarungi alimwambia Waziri Mkuu kuwa zaidi ya ng’ombe 2,000 wameibiwa mpaka sasa katika wizi huo.
Katika maeneo hayo yaliyokuwa na mauaji, Waziri Mkuu alifuatana pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema.
Akizungumzia Siku ya Serikali za Mitaa, Waziri Mkuu alisema kuendeleza kwa pamoja sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, ndiyo njia pekee ya kuondoa umasikini nchini.
Waziri Mkuu alisema kuwa kuanzia sasa, uongozi bora wa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti wa Halmashauti na Wakurugenzi, utapimwa kwa jinsi wanavyohimiza na kusimamia kwa vitendo kilimo, ufugaji na uvuvi.
Alisema viongozi waonyeshe uongozi wao kwa vitendo huko vijijini na siyo kukaa ofisini tu mijini.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumatano Julai 1, 2009
– – –
Date: Wed, 1 Jul 2009 09:36:53 -0700 (PDT)
From: Yona F Maro
Subject: Tarime, Rorya kutawaliwa kijeshi
Date: Wed, 1 Jul 2009 21:58:49 -0700 (PDT)
From: Japhet Makongo
Subject: Re: Tarime, Rorya kutawaliwa kijeshi
Suala la Tarime na Rorya linatia uchung na aibu. Hebu tushikamane kulitatua haraka.
Changamoto ya serikali katika kuthibiti vurugu zinapotokea mahali ni kukimbilia kuzima milipuko badala ya kuangalia kwa kina visababushi mahususi. Kauli ya Mh. Pinda kuwa sehemu za Tarime na Rorya zinaweza kutawaliwa kijeshi ni uamuzi ulio katika fikra hizo hizo za kuziba milipuko na ushahidi kwamba viongozi hawajafahamu tatizo la mkoa wa mara hususani wilaya hizi mbili. Sidhani kama utawala wa kijeshi (bunduki na mabomu) unaeza kumwongezea mwananchi kupata kipato cha kukimu mahitaji yake kifamilia ila una hatari ya kuchochea uvunjanji zaidi a sheria na kuhatarisha amani zaidi.
Maoni yangu ni kuwa tatizo la wizi, uvamizi na vurugu hizi limejikita katika “umaskini” Mwalimu Nyerere aliwahikusema katika moja ya busara zake kuwa “pengo kati ya wali nacho na wasio na walio nacho linapoongezeka, kwa hakika milipuko ni lazima” Na hapa nakubaliana na Mh Pind kuwa nguvu ya viongozi iwekwe katika kuimarisha uchumi wa familia katika kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara, badala ya kutafuta mchawi wa vurugu kisiasa.
Ningeishauri serikali itulie na kusaidiana na wananchi (viongozi wa kisiasa wameshindwa) kutambua tatizo liko wapi. Vyombo vya habari na hasa “Press Clubs” zina nafasi kubwa ya kutafiti kwa kina hali ya maisha ya watu wa tarime, musoma na rorya na kuandaa makala za uchunguzi utakao habarisha serikali na jamii hali halisi na kuwezesha kuchukuliwa hatua za muda mrefu. Aidha, Asasi za Kiraia zinayo nafasi nzuri ya kuishauri serikali matatizo wanayo yaona kwa jamii bila kujenga lawama na kunyoosheana vidole kuwa huyu kashindwa. Muda huu wa kukaa pamoja na siyo kukwepana kama inavyoonekana katika kushughulikia matatizo yanayojitokeza kamayale ya nyamongo. Busara inahitajika sasa.
Changamoto ziangaliwe katika umiliki na matumizi ya ardhi, njia mbadala za uvuvi endelevu (badala ya kung’ang’ania kuchoma makokot tu), matumizi ya raslimali zingine na hasa uchimbaji wa madini mdogo.
Media council isaidie kuwapa uwezo jopo la waandishi wenye maadili
Makongo
———————————————-
Japhet Maingu Makongo,
Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971
Dar es Salaam,
TANZANIA
suala la RORYA na TArime kwa ujumla imekaa kisiasa zaidi. nashanga\z waziri mkuu anaposema kuwa ataweka majeshi ambayo itakuwa inalinda usalama wa raia je atauweka lini wakati raia wasio na hatia na watoto wadogo w2anaendelea kufa? kwa nini hatujifunzi kutokana na yale tuliyoyaona rwanda? namuomba waziri mkuu aache siasa naamini kuwa ni mtekelezaji mzuri wa kazi za serikali lakini kwa hli anachelewa kuokoa maisha ya hawa waang wa vita vya kiabila.Hata hivyo ubaguzi wa baadhi ya kanda inadhihirishwa sijui kam ingekuwa ni kule kwao RUKWA angechelewa na kuendelea kuona mauaji kama haya.ni dahahiri kabisa kuwa amepotoka kwa hili na nianamuomomba ajue kuwa maisha ya watu yanaendelea kupotea. JOLUO WANABAGULIWA WANAONEKANA KAM,A SIO RAIA WA TANZANIA NA WANAFIKIRIKA KUWA WANAISHI KENYA TU,. mimi nafikiri baba wa taifa angekuwa hai angelaan ktendo hiki ca kuona vita,. aliwapenda watu wote na hakusubiri maauaji kama hayo yawe makubwa hivyo. nashauri serikali ichukue hatua ya haraka na si kusubiri.