Re: Barabara iliyozinduliwa kuwekwa LAMI inageuka kuzindua ajaili mbaya

From: Hildegarda Kiwasila
Date: Aug 7, 2009 2:40 PM
Subject: Re: Barabara iliyozinduliwa kuwekwa LAMI inageuka kuzindua ajaili mbaya

Yona maro ulichosema cha kuchukua hatua kwa wenye gari umefanya vizuri. Kama usingepeleka taarifa huko juu mbali mbali paolisi wa Ubunge wangekula hela basi. Mifano mingi ipo. Kama walivyosema wengine, ukimwambia dereva apunguze mwndo wenzako wanakuambia shuka wewe sisi tunataka kuwahi. Na unaweza ukashushwa mbali na DSM au na unakokweda porini kwa jeuri wakasimama ushuke na wakakurudishia pesa zako. Hivyo utaona, gari inakwenda kasi, na ndani yupo mwanajeshi au askari polisi hata trafiki kapewa lift au anasafiri. Kwa unyonye wetu, naye utamwona anakaa kimya anaogopa kushushwa. Au, dreva anaweza kupunguza mwendo kabisa akatembea 20 km kwa saa si umesema apunguze mwendo? Mle ndani wakaanza kukuzomea eti ‘unaona sasa dereva kakasirika amepunguza mwendo sana tunachelewa?’ Ila, ikipinduka kila mtu atasema dereva alikuwa anakwenda mbio. Sijui ni utaahira au vipi. Ikifungiwa leseni kutokana na ajali, tajiri anabadili jina la bus na kampuni anaendelea na biashara. badala ya Tawfik, inakuwa Tawakal na tutaipanda. Ukitaka kitu kifanyike ufike kwa mkubwa zaidi. Huku kwa akina sisi rushwa tupu, juu ufisadi hata kwenye roho za watu. Bado hata sisi wenye inakuwa kama akili zetu zina mushkel. Kila wakati boti za kienyeji zinazama ziwa victoria kutokana na kujazana sana katika boti. pamoja mtu anaona mtumbwi au boti inajaa, anaingia na mizigo inashehena mpaka wanazama. Na inatokea si mara moja. Hivi kujilina uzima na afya ni kazi ya serikali au ya nani? Ndio MV Bukoba ilivyozama, walipokataliwa kituo kimoja, wakaenda kupanda cha mbele ikawa balaa. Mimi nimekwisha kusimama katika ndege ninatokea Mwanza kwenda Dar. Nimepanda wa mwisho kwa kuwa nilikuwa nimebeba vitu mikononi wao walidhani mwenyekiti hicho haji tena. Mimi ninaingia mtu wa mwisho kiti kimeuzwa kakaa mtu waliomuingiza ili wambananishe na kiti cha mtoto ili mtoto apakatwe. Lakini boarding card ninayo na lilikuwa mstarini katika kuingia, kiti kimekaliwa. Nikaamua kusimama na mizigo kuwakomoa tu kama kwenye daladala. Ikabidi Air hostess anipishe kiti chake maana hela wamekwisha kula za watu waliowaingiza. Wao wakabaki wanachuchumaa landing na take-off hadi Dar wamesimama. Watu wanapakata watoto wakubwa wa kukaa katika kiti chao pekee. Uzito unakuwa mkuwa lakini ni unethical hata kama uzito si mkubwa. Viti vyao tumekalia mimi na mtu mwingine waliyemuuzia. Ikiwa abiria mmoja kwenda na kurudi ni laki 2 au 3, wakifanya hivyo kutwa au wiki nzima wana milioni ngani wanazogawana? Ni hatari na hiyo ni ndege kubwa private sio ya serikali kama ATC ambapo serikali ingelaumiwa. Private sekta nayo ina rushwa, umangimeza na ufisadi kama sekta za serikali. Hapo ninaambatisha picha ya watu ndani ya mtumbwi wenye engine au boat ya kienyeji yenye tanga na engine niliyopiga mwenyewe tulivyojazana mpaka watu wanasimama majini baharini hakuna anayetaka asubiri iende irudi mwendo wa dakika 10 kutoka Utende main Mafia Island kwenda Chole kisiwa kingine kidogo. Mtu upo kazini unawahi mkutano inawajibika kujazana hivyo na mzungu wetu tumemvalisha khanga na kilema kuzingatia mazingira. hatari tupu. Tunachezea uhai. Ukiwa una low pressure inapanda inakuwa hai pressure hasa unapokuwa hujui kuogelea ndio pressure inapanda- pressure inashuka. Ukerewe Island wanakufa majini mara kwa mara kutokana na ujazo. Train zetu zinajaza balaa.

From: Yona Maro
Sent: Friday, 7 August, 2009 20:09:13
Subject: [wanabidii] Re: Barabara iliyozinduliwa kuwekwa LAMI inageuka kuzindua ajaili mbaya

Ndugu Joseph

Ni wajibu wako wewe mwananchi kuhakikisha Unalinda usalama wako na wengine popote ulipo katika hili tuongelee katika vyombo vya usafiri , ukiona gari limejaza kuliko uwezo wake mkatalie dereva kuondosha gari hilo kama akiendesha kwa nguvu hata kama umelipa kituo kinachofuatia shuka ( ukiwa na tiketi ya basi husika na namba za gari hilo ) nenda
karipoti suala hilo katika vyombo husika ,unapofika pale kumbuko kunote jina la askari uliyemwambia suala hilo na namba yake ya shati kama amevaa uniform na chukuwa mawasiliano yao ya karibu kama namba za simu zao ,unatakiwa unote vitu hivyo kama chochote kikitokea huko
mbele kuweza kufuatilia vizuri kutokana na taarifa ulizotoa , naamini ukitoa taarifa hizo mapema askari polisi wanaohusika na usalama wa barabara wanaweza kulifanyia kazi suala hilo haraka zaidi usiporidhika unaweza kuwasiliana na wakuu wao ambao mara nyingi namba zao ziko katika vituo hivyo kama kote huko nakala ya lalamiko lako unaweza hata kuliweka hapa kwa wanabidii , nitaweza kuona ujumbe wako utafikishwa
kwa wahusika baada ya dakika chache tu .

image of the boat
Mjazano Kwenye boat Utende-Chole Mafia Aug 2008 Hilda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *