Re: Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania

From: Oppi, Igolola (Bulyanhulu)
Date: Aug 9, 2009 5:50 AM
Subject: Re: Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania

Ndugu wanabidii ningependa kuuliza tena kwa mara nyingine kuwa ushahidi
wa hili suala upo???, kwa sasa naona linaelekea kupotea wakati ni suala
la kizalendo na ni la kuwaokoa wananchi wa tanzania, hepu toeni ushahidi
wa hili ili tuweza kuona kipi kifanyike na msakabari wa ofisi za Bunge.

—–Original Message—–
From: bwiko.n@ . . .
Sent: Thursday, July 30, 2009 4:13 AM
Subject:Re: Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania

Kudadadeki you just opened my eyes……….I hope you have proof.

Those are some serious allegations there.

Cheers,

Bwiko.

——Original Message——
From: Leila Abdul
Subject: [wanabidii] Re: Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania
Sent: 29 Jul 2009 9:17 PM

KABLA YA HIYO KULIWAHI KUWA NA

Ama kweli, ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Kama unadhani
vigogo wa EPA ni mafisadi peke yao, basi ulikuwa hujamfahamu Spika wa
Bunge SAMUEL JOHN TEGEZA SITTA ! Ukimsikiliza anapoongea unaweza kuamini kwamba kiongozi huyo wa Bunge ni msafi kutokana na umahiri wake wa kujivalisha sifa kemkem – Mr Misifa. Unakumbuka hivi karibuni alivyomtukana Naibu Spika eti hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha mwenzake mbele ya umma, halafu bado anaendelea kuliita Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!

Tumebaini kwamba Sitta amekuwa akijimiminia sifa nyingi ili kulinda
ufisadi anaoufanya usigundulike katika jamii yetu. Ngoja nikupe tone tu
la madhambi yake kwa umma ili uone ni hatua gani utachukua, na ili na
yeye ajipime kwa nafasi yake. Angalia uchafu huu:-

– Anatumia vibaya fedha za umma. Amekuwa akitumia msaidizi wake kuchota mapesa kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi. Kila safari ya siku moja ndani ya nchi huchukua shilingi Milioni
tano (5,000,000/=), na kila safari ya siku moja nje ya nchi huchukua
shilingi Milioni Kumi na Tano (15,000,0000/=). Ameshindwa kufanya
marejesho ya masurufu (imprest) hayo, licha ya kupeleka risiti kadhaa za
kughushi/za uongo kwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge. Mpaka sasa
anadaiwa jumla ya shilingi Milioni sitini (60,000,000/=) za masurufu.

– SITTA hupeleka risiti za uongo kwa Mhasibu Mkuu, zikionesha madai
kutoka Oysterbay Pharmacy ya Shilingi Milioni Mbili ( 2,000,000/= )
aliyotumia kwa tiba kila wiki.

– Amekuwa akilazimisha hawara yake wa Hospitali ya Aga Khan naye alipwe posho kama wabunge anapokwenda naye Dodoma. Kwa mfano, hawara huyo alilipwa ‘per diem’ kuanzia tarehe 13/12/2007 hadi tarehe
31/01/2008 ( Siku 50). Huo ni Ufisadi mkubwa!

– Anaye kimada wake mwingine anayekwenda kwa jina la ASIA ambaye anaishi nyumba Na. 111 karibu na Mahakama ya Ardhi Upanga na amezaa naye. Huko mtaani kwao kimada huyo hujiita mama SITTA, na ni dada yake aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa iliyokuwa Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mwanamke huyo muda wote hutumia gari la Ofisi ya Bunge STK 232 Toyota RAV 4.

– Pia anaye kimada mwingine (jina limehifadhiwa) ambaye anaishi
kinondoni ( Livingstone), mtaa wa Honolulu katika nyumba ya kupanga
inayomilikiwa na dada yake Kawawa. Nyumba hiyo inatazamana na Nyumba Na. KH.MK/No. 337 katika mtaa huo huo. Kimada huyo hutumia gari ya kiofisi ya Spika mwenyewe STK 3002.

– Vimada wote hao hupata huduma za maji na umeme kwa gharama za Ofisi ya Bunge. Kuna kipindi mke halali wa Spika, aliwahi kulalamikia hali hiyo. Kuna siku maji yalikatika nyumbani, mke wa Spika akaomba apelekewe ‘ bowser’ la maji na Ofisi ya Bunge. Ohooo! Watekelezaji wakapeleka maji kimakosa kwa kimada. Mama Sitta akashtukia dili.

– Kuna taarifa kwamba mnamo Mwezi Oktoba 2007, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iligundua mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika SITTA. nimedokezwa kuwa Spika aliwanyamazisha wajumbe wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake hadharani!
Hapo inaonesha kuwa wajumbe hao walipewa rushwa!!

– Kama JK anataka viongozi wa kisiasa na wa serikali watenganishe
biashara na uongozi wa ku – ‘sacrifice’ kimojawapo, hilo litakuwa gumu
kwa sababu Sitta alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha
Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia ubia na
wafanyabiashara wengi wa Kigeni. Je, Wizara ya Maliasili na Utalii
inatambua kuwa Spika ana hisa kwenye kampuni moja ya Kichina
inayosafirisha nagogo licha ya marufuku yaliyowekwa?!

– Nililokupa hapo ni tone tu.

……………………………………..

SERIKALI IKAAHIDI KUMCHUNGUZA SOMA

Tanzania-daima-ijumaa-28-machi-2008

Sitta achunguzwa

na Happiness Katabazi

TUHUMA za ufisadi zilizosambazwa katika mtandao wa intaneti zikimlenga
Spika wa Bunge, Samuel Sitta, zimesababisha Ofisi ya

3 thoughts on “Re: Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania

  1. Jerome Shao

    Spika mstaafu Samwel Sitta akumbukwe kwa kazi iliyotukuka aliyoifanya ndani ya bunge la Tanzania.
    Alifanya kazi yake kwa kuzingatia misingi ya kiutu kwa maslahi ya Watanzania wote bila kujali dini kabila wala itikadi za vyama
    Wanaombeza spika huyu wametawaliwa na itikadi za vyama vyao na hawana uzalendo na nchi yao.
    ………………Tuwapuuze………………..

  2. johnson

    Huwo ndiyo ukweli.Kimsingi tukianza kufuatilia na kumchambua mtu mmoja mmoja,hakuna asiye fisadi hata viongozi wa dini.Kila mtu lazima anafanya ufisadi kwa namna moja ama nyingine.

  3. Jerome Shao

    Kwani Watanzania wote ni wanasiasa?
    ikiwa hujui kusali,na katika harakati zako za kumuvu hapa na pale ikatokea siku moja ukakutana na mtu” yuko njia panda anahubiri na mwilini amevaa nguo chafu na mbaya zaidi hajavaa Viatu mguuni,” usimdharau na kumnyooshea kidole! huenda katumwa na Mungu kukuwakilisha wewe usiyejua kusali.
    SERIKALI ISIWANYOOSHEE KIDOLE WANAOTAKA KUANDAMANA, WAANDAMANE KWA MASLAHI YA WENGINE WASIO NA NAFASI NZURI YA KUANDAMANA KTK KUTETEA MASLAHI YAO YANAYOPORWA NA MAFISADI WACHACHE!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *