Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

From: Rehema Kikwete
date Oct 30, 2009 9:28 AM
subject Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Taarifa na tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba vijana wengi eneo la afrika mashariki wanashiriki katika matendo ya ngono bila kinga yoyote kwa sababu ya tabia iliyojengeka katika jamii kwamba akinunua kinga anaweza kuchekwa au kuonekana ni mpenda ngono ana tabia chafu na maneno mengine mabaya mbele zao

Lakini kuna tatizo gani katika kununua kinga hii ya kumlinda maisha ya mtu dhidi ya magonjwa ambayo anaweza kupata kutokana na Ngono isiyo salama ? Kwanini vijana wanaona haya kununua kinga hizi ? kwanini wanafikiria ubaya tu wanaponunua kinga ?

Je wewe mwenzangu kama ni kijana huwa unafanya nini ? Nawe ni mwenye aibu kama wenzako ? Tatatizo ni nini haswa ?

– – – – – – – – – – –

From: Yona F Maro
date Oct 30, 2009 12:20 PM
subject Re: Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

suala hili la vijana kuogopa kutumia vifaa hivyo ni tatizo la kijamii jamii yenyewe haijamua kuamka na kuamua kupambana na ugonjwa huu katika kuanzia katika ngazi ya familia na zingine , hivi ni wangapi huko majumbani kwao haswa vijana hawa huwa wanakaa hata na wajomba zao , baba zao wadogo au wazazi wao wenyewe kuongelea mambo ya kawaida tu yanayohusu mahusiano ? ni wachache sana wengi wanafikiri kuongea na mtoto wake masuala haya ni aina Fulani ya kupotoka kwa maadili .

Mimi pia nimekulia kwenye mazingira kama haya sema tofauti ni aina ya shule nilizosoma na aina ya watu kwa kipindi cha sasa haswa humu mitandaoni tunavyo badilishana mawazo na kuchangia mambo mbalimbali nimeweza kujifunza mengi sana , kubadilika baadhi ya vitu na hata mwenyewe nimeweza kufunza baadhi ya vijana wale ambao nina bahatika kukutana nao mitaani au vyuoni humu .

Na mwisho nina mpenzi mmoja tunaaminiana , masuala ya afya yetu ndio nguzo ya maisha yetu ya kila siku na huwa tunaongelea masuala yanayohusu haya kama tukionana kwenye chat , au kwenye simu na hata tunapokutana ingawa tunaishi mbalimbali .

Naomba niishie hapa yasije kuibuka mengine

– – – – – – – – – – –

From: Rehema Kikwete
Sent: Fri, 30 October, 2009 17:28:25
Subject: Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Taarifa na tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba vijana wengi eneo la afrika mashariki wanashiriki katika matendo ya ngono bila kinga yoyote kwa sababu ya tabia iliyojengeka katika jamii kwamba akinunua kinga anaweza kuchekwa au kuonekana ni mpenda ngono ana tabia chafu na maneno mengine mabaya mbele zao

Lakini kuna tatizo gani katika kununua kinga hii ya kumlinda maisha ya mtu dhidi ya magonjwa ambayo anaweza kupata kutokana na Ngono isiyo salama ? Kwanini vijana wanaona haya kununua kinga hizi ? kwanini wanafikiria ubaya tu wanaponunua kinga ?

Je wewe mwenzangu kama ni kijana huwa unafanya nini ? Nawe ni mwenye aibu kama wenzako ? Tatatizo ni nini haswa ?

– – – – – – – – – – –

From: Hildegarda Kiwasila
date Oct 30, 2009 1:28 PM
subject Re: Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Ninachangia Kusema:

Wakati mwingine humkosea Mungu na kusema “Tumezaa sana kiasi kwamba vijana ni wengi vijiweni, hawafanyi kazi wapo wapo tu, wanakula bangi, pombe kisha ngono zembe, waache wafe au tufe tupunguze wingi wa watu”.

Elimu ya ukimwi imezagaa sana ila watu wanatunga mambo kibao ili kutimiza haja zao. Imani nazo za kienyeji hutumaliza.

Tufahamu kuwa-mwingine ambaye ni positive atakusaka au kumtafuta mpenzi wako, mwanao amuambukize kwa makusudi akuletee kama kukukomoa. Tujiongeleshe majumbani na wenzetu tuweke tahadhari na kujilinda.Wamama na wababa tuache tamaa. hata ajira sasa inabadilika ni kutoa ngono bila kinga.

Imani potofu na Uzushi
Mtu anaanza kuzusha kuwa wazungu wameweka vidudu ktk condom ukitumia utavunjika mwili wako hautakuwa rijali yaani athari ni kuwa sio mwanaume (ashakum hanithi) baada ya kugusana na hiyo grisi ktk condom. Huu ni uongo.

Tunafundisha vijana wetu ila wabishi na wakifika nje ni wepesi kufundishana na wengine mambo ya uongo. Peer group influence huingilia na kubadili elimu na mitazamo. Wengine wanasema wasichana wenyewe hawataki condom.

Kuna maeneo kweli kondom hazipo kiasi kwamba watu wanakodisha, unatumia, inakoshwa anatumia mwingine au wanatumia mifuko laini myepesi ya plastiki inawekwa hidi ndani ya vyumbani lodging. Lakini, sehemu nyingi sasa condom zinapatikana na zinauzwa shs 100. Wengine hata hiyo shs mia hana na haachi zinaa. Hata kama ameoa au ana mtu wake wa kudumu. Bado anakwenda nje.

Condom inasaidia sio kwa kuzuia ukimwi tu, hata maradhi mengine ya zinaa na uchafuzi wa njia ya uzazi kwa wanawake na wanaume fungus za aina mbali mbali na magonjwa ya zinaa. Na kama hayatibiki vizuri yanaleta utasa, virus na cancer, kuzima mkojo wanaume n.k. wanayojua madaktari.

Imani potofu ni nyingi. Hata sasa watu wanaamini mengi pamoja na haya hapa ambayo wengine tumekutana nayo ktk kazi zetu:

-Kondom itabaki ndani kwa mwanamke itakwamia huko na kupanda ktk mapafu na kuua. Kuna maponomu ambayo ni transparent ya kufundishia kuondoa dhana hii.

-Ukitumia kondom ina maana humpendi mpenzio unamuona mchafu. Wanawake ni wa kwanza kukataa kondom eti unamuona najisi-mchafu. Kila mtu ana uchafu wake na unapochangia mke au mume ni kwamba hata kama si ukimwi unaupata huo uchafu wa fungus, viral etc,

-Mapenzi kwa kondom ni sawa kama kula pipi ikiwa ndani ya mfuko wake wa plastiki, kwanza ni kumdharau mwenzio kumuomba avae kivalo hicho na kivalo kinaathiri mapenzi.

-Mwanamke kudai kondomu au kuwa na ile kondomu ya kike kuvaa yeye ni dalili kuwa ni malaya au sio muaminifu. Baadhi ya wanawake wameua wanaume kwa kukuta condom ktk suruali yake.

-Kuvaa condon ni kutangaza uuaji. Unaua watoto kabla hujawazaa unawazika. Imani hii ya kuzika watoto kabla kuwazaa imezagaa machimbo ya madini ambako sex bila ya kondomu ni bei ghali (inalipa zaidi) kuliko kwa kondom. Kuna mabada ya muda mfupi yamezagaa ktk madini na changu doa mgini anapigwa mnada kwa hela ya juu watu wanamshindania. Mwenye dau kubwa ndio anamchukua. Kesho mwingine tena anamchukua.

-Kondomu linaumiza, linaathiri kuridhika kimapenzi. Ina maana utaalamu wote unaisha kama kuna condom, hakuna mapenzi ila ni kondomu.

-Unatumia condom kwa mtu usiyemjua, mkisha kutumia mara 1 hadi 3 na mkiisha kuzoeana basi-mnajuana, mmezoeana hakuna haja, mnaaminiana. Hata kama kati yenu mmoja ni positive-mmekwisha kuzoeana.

-Ukiwa umeolewa au umeoa-kondom haina haja ni mke au mume wa mtu umeolewa hivyo msafi huna wadudu au maambukizo.

-Una madigrii-msomi uwe wa chuoni, ofisini, hospitali etc mradi tu msomi huna HIV au kuwa na uezekano kuwa unao. Hivyo-unawapata tu ukiwa unaitwa Dr, Professor, Mkurugenzi, Daktari etc-immune huna

-Sura nzuri, mtanashati unanukia, mrembo, handsome, unajulikana kila mtu anapenda uwe karibu naye unatajwa kila unapopita.

-Mnene hujakonda na ni juzi tu mkeo kajifungua mtoto na wote wazima.

-Ukinawa tu mara baada ya tendo wadudu wa ukimwi hufa au ukinywa maji baridi mara.

-Tendo la ndoa kinyume na maumbile halisababishi ukimwi hivyo hakuna haja ya condom

-Msichana virgin hana HIV-anaweza kuzaliwa nayo ila haijajitokeza

-Watoto ni salama hawana HIV-ndio maana ubakaji wa watoto na wasichana wadogo umeongezeka. Ambapo anaweza akazaliwa na HIV au unakuwa nao wewe unadhania ndio utatibika kwa kuwa naye-Imani potofu kama ile ya kuua albino ili utajirike.

Haya ndio baadhi ya maelezo tunayokutana nayo kwa vijana tunapowafundisha masuala ya ukimwi. Ni tatizo kwa watu wazima pia kwa sababu walio wengi hawaufahamu vizuri mfumo wa uzazi, wanachokielewa ni kinyume chake

Tuangalie pia, tusikazane na vijana tu, tukazane na wanaume hasa watu wazima ambao wasichana wakishindwa maisha, hurudi vijijini ambapo wanakosa pa kuishi na kuwavamia vibabu katika vibanda vyao na kuishi nao kwa vile wapo pekee au wana mali nao hawana kitu. Vibabu vikilewa pombe vilabuni vijijini vinachukua changu doa wa vijijini na hawataki kushindwa kutukana kuitwa wazee eti zao zimekwisha. Wazee husema hivi kuwa hawapendi kuambiwa ‘wewe babu zako zimekwisha kama bado njoo tuone!!’ huu ni ujinga hawa nao kwa sasa wanapanda chart juu ya HIV na hawaielewi vizuri.

-Akina baba na akina mama ngariba wa kienyeji wameonekana kupanda chati ya HIV positive
-Akina mama wakunga wa Jadi wanaozalisha vijijini wanaambukizwa kwa kuhudumia wanawake, watoto wao na jirani kuwazalisha bila ya tahadhari au gloves.Kumzalisha mtu kwa gloves eti unamnyanyasa. akiwa mwanao ana HIV analia eti una mnyanyasa unamshika kwa mipira. Unamkosha mzazi (mwanao) ila ana matatizo nawe una michubuko.

-Waganga wa jadi wanaochanja wagonjwa baadhi wanaukimwi na wanajikata au kunyunya damu wanaita ‘kupiga chuku’ au wale wanaofanya dawa ambapo anachanja mgonjwa ila kumpaka dawa anaweka katika utupu wake na kumpaka (waganga wa Kimakonde-wamawia ndio wenye uganga wa aina hii). Pia kuna waganga wanaozini wateja wao wa kike kwa tamaa. Mke anajua ila ndio analinda ndoa maana mgonjwa yupo hapo muda mrefu anatibiwa na hana hela ya matibabu. Hiyo ndio fidia.Kumbe anaumwa hayo maradhi ya magonjwa nyemelezi yatokanayo na HIV.

-Polisi wanaokamata changu doa mijini hupewa rushwa ya ngono ili kuwaachia. Hawa wamepakatika na kuathirika sana
-Wageni wajao majumbani na watoto wako ktk kuchangia vyo vyombo kama wana TB na wengine ujinga hupigia miswaki ya watoto au kumegeana vitu kwa meno na watoto wadogo wanaoombaomba akiona mtu anakula.
-Watu/wazazi kuachana halafu kurudiana bila ya kupima eti nini ni Mzazi Mwenzie.

Bado kazi tunayo kuelimisha jamii. Akili zetu zinaonekana kushukia zaidi chini ya miili yetu kiasi kwamba, mawazo ya tamaa ya kimwili yamejaa wakati mwingine yanaziba yale halisi yote uliyoyaona ktk mazingira yetu na tulivyoona jinsi baadhi ya familia zilizoathirika, zinavyoteseka; uliyemzika alivyoteseka, jirani, ndugu au rafiki aliyekuwa HIV positive alivyopata tabu. Unajiona wewe hautopata-upo mwangalifu, mchaguzi mzuri na muangalifu ila-hutumii condom na huachi kuchanganya changaya.

– – – – – – – – – – –

From: Samson Hayuma
date Oct 30, 2009 6:04 PM
subject Re: Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Swala hii la watanzania kuogapa kununua kinga kwa sababu et watachekwa na jamii.,Ni kwa sababu aslimia kubwa ya familia za kitanzania bado wanafua mambo ya utamaduni,mila na kathalika. Pamoja na kuelimishwa kila kukicha bado hatusiki kabisa et tuna mcheka mtu kama ananunua kinga kwa afya yake!? Tubadilikeni jamani vinginevyo tutaendelea kupiga kelele bila mafanikio.

Sijawahi kuchekwa na mtu. Mimi sijaowa siku nikiwa na ahadi na rafiki yangu wa kike huwa tuna mpigia simu Doctor wetu na kumweleza saa ngapi tumwende ili atupe kinga na ushauri zaidi jinsi ya kutumia silaha huo.

Dada Rehema na wanabidii: Tatizo ni kwamba hizo kondom zinauzwa kama karanga mitaani na watu wasio wataalamu wa kazi hizo. Tasisi husika watabidi watoe elimu kwa wale wote wanao uza kondom.

– – – – – – – – – – –

From: Hildegarda Kiwasila
date Oct 30, 2009 8:19 PM
subject Re: Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Kwanza afadhali ya vijana wana mitandao mingi ya kununua kondom kuliko wazee. Hawa ndio wana aibu zaidi.

Inasikitisha sana. Wakati wanajenga mradi wa umeme wa Bwawa la Kihansi, tulikuta condom maboksi kibao. Toka zitolewe kwa mradi wa kupunguza athari na makali ya mradi kijamii ktk maradhi ya kuambukiza yanayoweza kutokea, condom hazikugawiwa. Unazitambua kwa alama ya rangi ya cover yake. Villlage health workers walikatazwa na kamati ya kijiji kugawa condom eti zinaongeza umalaya. watumishi ugani tena wana nguvu gani juu ya wazee wakijiji!!

Yet, ktk matatizo makuu ya kijijini mojawapo lilikuwa ni maradhi yasiyotibika kwa dawa za kienyeji hadi waende rufaa Health cEntre, hospital (Kaswende, kisonono etc). tatizo lingine lilikuwa kuibiwa wake na wachumba zao na wageni waliokuja kuchimba na kujenga bwawa (baadhi toka nchi za nje wenye fedha hawana wake); wale waliokwenda Kihansi kutafuta vibarua wanahanja vijijini na baadhi ya waajiriwa from within TZ ambao nao wanauwezo hawakuhamia na wake au familia zao ktk kujenga mradi haujakamilika.

Kesi number 1 faili la kata ktka mashitaka-kuvunjika ndoa, uchumba na talaka, zikifuatiwa na wizi mashambani ambao ulikuwa ni mgeni ukifanywa na waliokuja kutafuka vibarua na kukosa wanazurura vijijiji; ubakaji ulikuwa mgeni pia.

Nilipowauliza wazee kama hiyo condom wanayosema inaongeza umalaya/uzinifu kwa akina mama na ina madhara pia jee kuna mtu ameshawahi kuona hiyo kitu. Anyooshe mkono ambae anaijua na ameshaiona. walinyoosha sio zaidi ya 4 nao walikuwa ni walimu na watumishi wengine waliohudhuria kikao hicho. Ambao hawajaiona wanyooshe mkono-UKUMBI MZIMA wa WAZEE wa Kijiji cha Uhafiwa (mwaka 1997 Bwawa likijengwa). Nikawauliza kama wapo watu wanaotaka kuiona Condom-wakanyoosha mikono wote ambao hawajaiona. Nikawatolea baada ya kuwataka radhi kuona hicho ni kitu gani wanachokiogopa. Kwanza wengi walikishangaa kuwa ni kitu si cha maana kiplastiki kidogo tu. Baadhi walicheka kabisa na kutingisha vichwa. Ila, kutokana na wazee wa mila kushika bango VHW wasigawe n.k wakawafanya wenzao waamini kuwa hicho kitu ni cha hatari ila hawaelewi kipoje. Na ukiwauliza Condom inafikaje ktk mapafu na kuweza kuua mwanamke-maelezo ni uongo mtupu.

Mradi wa uhamasishaji kuhusu Social impact of Kihansi Dam -upande wa afya (Chini ya NORCONSULT-MUHAJAKI) ulianza na matatizo haya, uliathirika na STDs zilikuwa high kutokana na VHW kukatazwa kugawa condoms. na hivi ndivyo wanavyopakatika sasa kote kulikokuwa na miradi ya mabwawa ya umeme, mabarabara na mengineo. Machimboni ya madini ndio balaa.

Tukaeleweshana madhara yote ya kuto kutumia hiyo plastiki nao wana wake zao (katika ndoa zao) zaidi ya mmmoja (pamoja na kuwa zaidi ya 90% ni wakristu); tatizo la kumlazimisha muhudumu wa afya azingatie mila badala ya mafunzo aliyopewa, kuzuaia akina mama wasile dawa za uzazi (watazini hovyo, ukristu unakataza). Ni matatizo makubwa sana. Makanisa yanazika waumini kutokana na HIV ila yanakataza kondom.

Ni vizuri ktk kufundisha vijana na wazee kutumia hiyo condom kuwaonyesha na mabonomu ya kuonyesha jinsi ya kuvaa. Hearsay ni mbaya sana. Na siku hizi zipo za me na ke. Lakini tathimini za miradi hii ya HIV na kondomu matokeo yake yanasikitisha.

Sasa itawezekana kweli Samson Hayuma kwenda kwa daktari kila mara unapotaka kuonana na bibie ya ukweli hayo? Ila, inafaa sasa kulindana, kama unajiona unapitepite nyingi, mlinde mwenzako nyumbani basi angalau mmoja abaki kuangalia familia. Usitake peku peku nje na nyumbani peku pia. Kwa Mungu sijui utakwenda kusema nini maana unaua kwa makusudi.

One thought on “Kwanini Wanaogopa Kununua Kondom

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *