from Ulanga Ally
date Nov 14, 2009 6:59 AM
Tetesi toka vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa Dr Slaa anatafakari
kugombea urais kutokana na shinikizo toka kwa wananchi ndani na nje ya
chama chake.
Habari zinaeleza kuwa hata uamuzi wa viongozi wakuu wa chama hicho na
wabunge kufanya kikao cha pamoja Dodoma ilikuwa ni sehemu ya hatua
kuelekea maamuzi hayo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati CCM ikifanya kikao na wabunge wake
Dodoma na Kamati ya Mwinyi, wakati huo huo kikao cha Mbowe na wabunge
wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kilikuwa kikiendelea.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kambi ya Lowassa na Rostam Aziz kupata
taarifa hizo sambamba na kikao cha kawaida cha kuidhibiti kambi ya Sitta na Malecela palifanyika kikao cha kuidhibiti CHADEMA na kuzima azma ya Dr Slaa kugombea urais kupitia chama hicho.
Mtoa habari wetu anaeleza kuwa katika kikao hicho iliamuliwa kama mkakati wa muda wa awali uwepo mkakati wa kuvunja imani ya wananchi kwa Dr Slaa kupitia kuvunja imani ya CHADEMA na utendaji wa Dr Slaa kama katibu mkuu.
Chini ya mkakati huo iliamuliwa kwamba magazeti ya Mtanzania na Rai
yaendeshe propaganda za kudumu yenye dhamira ya kuonyesha kwamba
CHADEMA ni chama cha udini, ukabila na ubadhirifu wa matumizi ya ruzuku. Kama sehemu ya mpango huo habari za mara kwa mara ziandikwe kumhusisha Chacha Wangwe na Zitto Kabwe na masuala mbalimbali
yanayojitokeza ndani ya CHADEMA.
Kwa upande mwingine, gazeti la Mwananchi ilikubaliwa kwamba liibue
suala la Dr Slaa kugombea urais. Tayari gazeti hilo katika toleo lake mojawapo la wiki hii limeshamtaja Dr Slaa kama mgombea urais wa mwaka 2010. Mkakati huo pia utahusisha kuhoji jitihada zote za Dr Slaa za kupambana na ufisadi zikihusisha na nia yake ya kugombea urais na kuelezea vita hiyo kuwa ni ajenda ya kusaka madaraka. Habari hizo pia zitahoji utendaji wa Dr Slaa ndani ya CHADEMA na kutaka aondolewe kama ambavyo kuna shinikizo la kutaka Makamba aondolewe kwenye nafasi hiyo ndani ya CCM. Habari hizo zitahusisha kuhoji baadhi ya watu na hata pale watakapokosekana habari zinazoitwa za kiuchunguzi zitaandikwa.
Mtoa habari anaeleza kuwa uamuzi wa kambi kuishughulikia CHADEMA na Dr
Slaa hautokani tu na ukweli kuwa Orodha ya Mafisadi iliyotolewa naye
Sept 15 mwaka 2007 bali unatokana na hofu kubwa ya ushirikiano wa kiajenda kati ya viongozi wakuu wa chama hicho na wabunge wa ndani ya CCM wanaojiita makamanda dhidi ya ufisadi.
Inatarajiwa kwamba mkakati huo utaweza kuzalisha mgogoro na makundi
ndani ya CHADEMA lakini pia utaleta mgawanyiko wa kiajenda ndani ya
chama hicho kama ilivyo kwa CCM. Kama mkakati huo ukishindwa kuleta
mgogoro ama mgawanyiko basi inatarajiwa walau mkakati huo utasababisha Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wake Dr Slaa washindwe kukiongoza chama hicho kutokana na mivutano ya moja kwa moja na hivyo chama kupoteza nguvu yake kinapoelekea mwaka 2010.
Chaguzi za marudio za Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo
ambazo kwa sehemu kubwa wagombea wake kwa upande wa CCM walitoka kambi inayoitwa ya mafisadi zimetoa ishara kwao kuhusiana na nguvu za
CHADEMA kwenye ngazi za ubunge kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Hivyo, namna ya kuvunja nguvu hizo ni kuhakisha chama hicho kinavurugika ama wananchi wanapoteza imani nacho mapema.
Tayari viongozi wakuu wa chama hicho wamekuwa na misimamo tofauti
katika hoja zinazohusu ufisadi hali inayoashiria kuanza kwa mpasuko wa
kiajenda katika chama hicho. Kwenye masuala hayo mbalimbali Mwenyekiti
Freeman Mbowe amekuwa na msimamo sawa na Katibu Mkuu wake Dr Slaa huku
Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe akiwa na msimamo tofauti nao.
Baadhi ya masuala yanayotajwa ni pamoja na kuingia kwenye Kamati ya
Madini(Bomani), hoja ya Mkapa kustakiwa, Mitambo ya Dowans, taarifa ya Kamati teule kuhusu Richmond na suala la Dr Mwakyembe kuhusu mradi wa kufua umeme Singida. Katika siku za karibuni viongozi hao wametofautiana kimsimamo kuhusu kutenguliwa kwa uteuzi kwa maafisa wa chama hicho David Kafulila na Danda Juju. Wakati Mwenyekiti Mbowe na Dr Slaa wametoa msimamo mmoja wa kupinga utovu wa nidhamu ya kiutendaji na maadili ya uongozi wa maafisa hao, Zitto amemtetea Kafulila pekee akieleza kwamba hatua hiyo imemwonea ikimlenga yeye na kwamba itaathiri nafasi ya Kafulila kugombea ubunge wa Kigoma Kusini ambapo yeye amemwandaa kwa muda mrefu kuwa mbunge.
Dr Slaa amekuwa akikanusha mara kwa mara kuwa hakusudii kugombea urais
na kwamba yeye anapendelea zaidi kuwa mbunge wa Karatu. Mwenyekiti wa
chama hicho Freeman Mbowe ambaye aligombea urais mwaka 2005 tayari
ameshatangaza kutogombea urais mwaka 2010 na ameelekeza nguvu zake kurejea bungeni kupitia jimbo la Hai ambalo ameliongoza mwaka 2000
mpaka 2005. Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe, yeye
ametangaza kugombea urais siku za baadaye. Wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa kwa umri wake, hatakuwa amefikisha umri wa kugombea urais mwaka 2010 hata hivyo anaweza kugombea urais mwaka 2015. Wachambuzi wengine wa mambo wanaeleza kuwa mvutano ndani ya CHADEMA kama ilivyo ndani ya CCM unaweza kutokana na nia za wanaotarajia kugombea urais mwaka 2015 ndani ya vyama hivyo.
– – –
subject TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Leila Abdul
date Nov 14, 2009 9:14 AM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Slaa kama akigombea urais angeweza kupata kama wananchi wangekuwa
wameelewa na kama vyombo vya usalama vingekuwa vinapenda mabadiliko.
Lakini kwa sasa inaonyesha bado vyombo vya usalama havipendi
mabadiriko kwa sababu maafisa wengi ktk idara za usalama ni vihiyo na
wala rushwa.
isack mchungu hide details Nov 14 (2 days ago)
reply-to wanabidii@googlegroups.com
date Nov 14, 2009 12:05 PM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
NGUVU ya ziada za ushirikishwaji uuma, umakini,uimara wa mawazo na misimamo ya pamoja vinahitajika kuhakikisha CHADEMA inakwenda bali mwaka 2010 katika uchaguzi l;akini kama mambo yatakwenda kama yanavyokwenda sasa kwa kweli bado itakuwa vigumu nadhani wote CCM tunaijua. Nyumba imara ndiyo inayohimili mikiki lakini nyumba yenye ufa haiwezi kuhimili hata siku moja bado itakuwa ndoto kuiondoa CCM madarakani,DR SLAA ok fine ni kiongozi safi na anaetegemewa lakini kwa mkondo huu wa CHADEMA inavyokwenda itakuwa hakuna kitu!! nawashauri chadema kama wanataka mambo yaende vizuri mwaka kesho hawana budi kuacha utoto wanaoufanya sasa hivi maana wakati wa kujipanga ni huu sio kugombana!!!!!
alfred nchimbi Nov 15 (23 hours ago)
date Nov 15, 2009 1:14 AM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Nimeisoma hii habari kwa umakini kabisa na nimeona mwandishi anataka wasomaji wapate picha kwamba Dr. Slaa ni tishio kikubwa kwa CCM na kwamba CCM wanafanya vikao kuona namna ya kumzuia. Mimi naamini Dr. Slaa ana haki kabisa kikatiba ya kugombea urais na kimsingi hatakuwa wa kwanza kufanya hivyo akitokea kambi ya upinzani na wala hatakuwa wa mwisho. Mwaka 1995 waligombea watu wanne Mkapa, Lipumba, Mrema, Cheyo na kama utakumbuka Mrema alikuwa amefikia umaarufu wa juu ambao hakuna kiongozi yoyote wa upinzani ameweza kuufikia leo hii. Pamoja na ukweli huu ilikuwa ngumu kwa Mrema kushinda lakini alipoomba ubunge tena kwenye jimbo gumu sana la temeke alipata kura nyingi na kuwa mbunge huko. Sasa iwapo Slaa anataka kugombea hilo ni jambo zuri kidemokrasia lakini uchaguzi wa serikali za mitaa umeonesha kuwa wananchi bado wana imani kubwa sana na chama cha mapinduzi. Kwa mfano, hata zile sehemu zilizofikiriwa kuwa ngome imara za CHADEMA pale kinondoni chadema
haijafikisha viti vitano. Kwa kinondoni licha ya kuachwa na CCM kwa mbali sana CUF imeonekana kuwa juu ya CHADEMA. Lakini pia kutokana na uzoefu wangu mdogo ndani ya chama napata shida kuamini kuwa suala la Dr Slaa linaweza kuingia kwenye agenda wakati vikao ndani ya CCM viko busy na mambo muhimu ya kitaifa. Kwamba Dr. Slaa anawaza kugombea urais mwakani sio issue kwa CCM. Kampeni na shamrashamra za urais kwa CCM sio za siri kihivyo. Wakati utakapofika utaziona hizo harakati na kama kuna mtu yeyote wa kubezwa utawasikia watu wakibeza wakati huo. Hiki ndio chama cha mapinduzi ninachokijua mimi.
Alfred
MANACE NKULI
date Nov 15, 2009 4:56 AM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Mmh! sie watanzania ni watu wa ajbu sana, tunaamini mambo kama vile hatuwezi kufikiri. Kila mwenye akili timamu anaweza kutambua kati ya Zitto na Dr. Slaa ni nani “opportunist” na nani anaongea kama mzalendo. Tatizo tunapenda watu wengine wafikiri kwa niaba yetu kama vile “wahariri corrupt”, n.k. Kama mtoa mada hapo chini alivyodokeza kuhusu magazeti ya Mtanzania na Rai hayo kazi zake zinajulikana, ni kweli hivi karibuni Mwananchi wameanza kunishangaza (ameanza andika KOMEDI) ila naamini jambo moja kwamba haitakuwrahisi kudanganya watu kama walivyowahi hapo nyuma, kwa sababu safari hii hata sie waelewa tunajihusisha na maedeleo ya siasa ya nchi yetu. Ushauri, waache fitina, badala waconcentrate kutekeleza ilani iliyowaweka hapo kama wanavyodai.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
“utpctz@ . . .
date Nov 15, 2009 6:04 AM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Si zitto si slaa hakuna haat mmoja mzalendo wote ni maopportunisti
Sent from my BlackBerry® smartphone from Zain Tanzania
Rehema Kikwete
date Nov 15, 2009 10:51 AM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Slaa ni chaguo zuri la urais lakini ana chance tu endapo ataungwa
mkono na kambi nzima ya upinzani, kitu ambacho sidhani kama kitatokea
kwa Tanzania yetu tunayoijua. Itakuwa ni pigo kwa upinzani in general
kama Slaa ataamua kugombea urais na kushindwa (which is more likely
kama CHADEMA itasimama peke yake) kwa sababu hatakuwa na nafasi tena
ya kugombea ubunge Karatu ambako anaonekana kuwa na nafasi kubwa sana
ya kutetea kiti chake. Ikitokea hivi maana yake ni kwamba kambi ya
upinzani bungeni itakuwa imepoteza kiti, tena cha mbunge muhimu kama
Slaa (arguably the most influential MP of 2005-2010). Ni muhimu sana
kuwa na strong opposition bungeni ili kujaribu kuinfluence utendaji wa
serikali kutokea mjengoni kuliko kukimbilia kuingia Ikulu bila strong
base ya wapiga kura. Let’s be realistic, kwa mazingira ya kisiasa
yalivyo sasa TZ ni vigumu kuona upinzani wakishinda kura za urais bila
kuunganisha nguvu.
Juma Mzuri
date Nov 15, 2009 10:56 AM
subject [wanabidii] Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
signed-by googlegroups.com
mailed-by googlegroups.com
Sure, hapa umeongea nukta tupu! Kumpoteza Dkt Slaa Bungeni ni pigo
kubwa mno kwa upinzania! Prof Lipumba na wapinzania wengine wote
watumie approach ile ile aliyotumia Seif kule Zanzibar alipomtambua
refarii (Rais Karume) katika dakika ya 88 ya mchezo, kwamba “tunafanya
hivi kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari.” Kwa hiyo wapinzania nako
watoe nafasi kwa Dkt Slaa ya kugombea urais na waseme kwamba
“tunafanya hivi kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania.” La sivyo Slaa,
usijaribu a loosing battle!
Amani Kerege
date Nov 15, 2009 2:46 PM
subject Re: TETESI – Dr Slaa Kugombea Uraisi 2010
Hii ndiyo jeuri ya CCM ya siku zote kama anavyoonyesha Alfred hapa. Ni vizuri wakajiamini hivyo lakini pia tunataka uchaguzi uwe wa haki usio na wizi wala ujanjaujanja. Najua nguvu yote ya dolka iko nyuma ya CCM na vyombo vyote vya serikali na vyombo vya habari vya umma vinafanya kazi kwa niaba ya CCM. Lakini hii pia ilikuwa hata huko Kenya na Zimbabwe na bado wakongwe wakadondoka. Siku CCM itakapodondoka mtabaki vinywa wazi.
Lakini haya masuala ya kitaifa mnayojadili ni yapi hasa? Maana sisi tunategemea kusikia matatizo ya umeme, ujambazi, ufisidi, huduma mbaya za afya, rushwa serikalini na katika vyombo vya sheria, miundombinu mibaya, Loliondo, huduma duni za maji, elimu duni nk. yakapewa kipaumbele na tukajua nini kinafanyika katika hayo. Sasa miaka 48 mnakaa tu kujadili mpaka leo hamjui mfanye nini? Mtajua lini?