Kuna Habari kupitia gazeti la Mwananchi kuwa Zitto ameweka bayana kuwa anataka kujivua nafasi zote kupitia Chadema kutokana na hali ya
kisiasa kupitia Chadema na kudai kuwa anataka kuendelea na maisha yake ya kawaida na pia amesema kuwa ataendelea kumuunga mkono mgombea wa NCCR MAGEUZI Kigoma Kusini hata kama CHADEMA wakiweka mgombea wao.
Je Ndugu zangu wadau wanasemaje huu ya hali ya mambo ndani ya CHADEMA.
Hali kama hii inakatisha sana tamaa na kuona badala ya kwenda mbele
tunarudi nyuma.
Tatizo letu siasa zetu bado ni changa sana kama ilivyo nchi yenyewe,
siasa inayoruhusu pesa za wafanyabiashara kufanya kazi yake ndiyo tabu
yake, mwanasiasa anaonekana ana msimamo mzuri akishaanza kuyumba yumba kwa sababu ya ushawishi fulani uwe wa pesa au wa namna nyingine basi
hatufai kamwe!!
misimamo mibovu ya watu wa aina hii inawachanganya wananchi na kuwaweka gizani kwamba waelekee wapi sasa!! maana hata wale wanaowategemea kuwaonesha njia muafaka wanajikanganya, HIVI KUNA SIRI GANI YA MIGOGORO NDANI YA VYAMA VYA SIASA VYA TANZANIA?
Hakuna sababu ya vyama vya upinzani Tanzania kwani elumu yetu katika demokrasia bado ni ndogo sana kuanzia kwenye viongozi waandamizi hadi kwa raia. Mfumo unaofaa Tanzania ni wa chama kimoja lakini wagombea wa Urais wawe watatu. Katika wagombea watatu lazima mmoja ana afadhali. Tunapoteza mda wetu kuwa na vyama vingi vya siasa.
Hilo la Barua Pepe zake kuangalia inawezekana sana kwa sababu kuna
mtu mwenye mamlaka na email zote zilizoko kwa majina ya chadema huyo
anayetengeneza hizo anuani na kadhalika , kuepuka mambo kama hayo ni
kwa wananachama na waajiriwa wa chadema wanaotumia anuani za majina ya
chama kuwa na mkataba kati yao na chama husika lakini vile vile ni kwa
wanachama wenyewe na viongozi kuangalia sehemu wanazotembelea haswa
kwenye viwanja vya ndege kwenye mahoteli wanapotumia computer za huko
kutembelea account zao za barua pepe inawezekana kuweka programu
zinazohifadhi kila anachoandika mtu kutumia computer hiyo na mtu
kutumia maelezo yaliyohifadhiwa kutembelea account husika akiwa sehemu
nyingine .
Na lingine ni kwa wanasiasa wa ngazi zote kuangalie mienendo yao
kwenye mitandao jinsi wanavyochangia mada na tabia zao kwenye
mitandao hii kwa faida zao na vyama vyao au kampuni wanazofanyia
kazi , kwenye nchi kadhaa sasa wameshaanza kuwa na mikataba kati ya
wafanyakazi na kampuni au mashirika yanayoelekeza jinsi wafanyakazi au
waajiriwa wa sehemu hizo watakavyochukuliwa hatua kama watavunja miiko
fulani pindi wanapowasiliana kwenye mitandao hiyo
Thanks. Kukata tamaa ni jambo baya kwani haina tiba wala kinga. Wakatoliki wanaita dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu sijui wenzetu wengine wanasemaje,
Kuingia na kutoka chama cha siasa ni jambo la kawaida. If anything ni kigezo sahihi cha kuwapima viongozi.
So sidhani kama kuna haja ya kurudi chama kimoja. Asiyeona manufaa ya vyama vingi hafanyi utafiti wa kina.
Ni muhimu pia kujua kuwa chama Taasisi ni kubwa kuliko personalities ndani ya vyama na tatizo ya wengi ni kujenga personalty cult. Tutakapofika kama wenzetu wa miaka 200 kwenye democracy these will no longer be central issues
Hata akiondoka sitashangaa mana amekua mpinzani ndani ya upinzani…mimi sio mwanachadema lakini zitto kabwe amekua na kauli nyingi sana zenye utata…mara anasema kuna tatizo ofisini kwa katibu mkuu ambayo yeye ni naibu!!! mara kafulila kaonewa, na mengine mengi…..kwa wale wenye kuelewa mambo vizuri tulishangamua huyu zito ana lake jambo..na anajua rohoni mwake…wala asisingizie eti kafulila kaonewa….huu ni mpango wa kuimaliza chadema na hautafanikiwa kamwe…
Ninaamini zitto hatakua mtu wa kwanza kuwasaliti watanzania hata kabouruou alisaliti akaenda ccm…orodha yao ni ndefu… lakini pia naamini bila zito upinzani unafanya kazi nzuri sana na pia hata akienda bado utakuepo…hatuwezi kukata tamaa eti kisa zitto anasema anajiuzulu…jiuzulu uende kwa amani na Tanzania yenye watanzania wenye uchungu na nia dhabiti ya kuitetea nchi hii wapo wataendelea kuwepo……ALUTA CONTINUA…
Tanzania ya leo imejaa vijana wengi waoga,wanafiki,walafi,na wanaozingatia matumbo…shame on us,…..kizazi cha hovyo kabisa hiki kisingemuondoa mkoloni kamwe!!!!
Tatizo ninaloliona ni la kwa nini Mbowe hajitokezi kujibu mengi
yanayoisulubu CHADEMA??
Inakuwaje watumishi na wanachama maarufu/muhimu (Kafulila & Danda
Juju) wanahama chama lakini mwenyekiti hajitokezi kutoa angalau tamko
au kujibu maswali ya waandishi wa habari?
Mbowe kama anaogopa waandishi leo hii kwa mambo madogo madogo kiasi
hiki, je anategemea kumuongoza nani?
Precedence may save us well. So, what did Mwinyi tell the press when Mrema bolted from CCM? How useful were any prouncements from CCM top echelon? What did the Chair say when the key CCM members who left to form the core of the opposition?
For that matter, what did the NCCR/TLP/CUF Chair say when Lamwai, Hiza, Rwekatare, Kabourou, Ngawaiya, et al bolted their parties? How useful would it have saved the bodypolitik?
My take on this is that individuals in any serious party are cogs in the wagon. They can leave, they can die, they can drop off and the general direction and speed of that party should not change that much. Perties that are based on a personality cult may be much more affected.
Jamani, Mwalimu alitutoka tuka-survive, ije kuwa katibu mwenezi au mwenyekiti wa chama? Party hopping for fundamental reasons is quite common and actually healthy. Sometimes the party becomes a straight jacket for a fast evolving member. Sometimes individuals acquire an inflated sense of self importance and seek a platform that can cater for their ego. Sometimes the party looses its compass and members will eject.
Kuna mtu atashangaa kama viongozi kadhaa wakitoka CCM kwa hali ilivyo sasa hivi? Does Kikwete have to say anythinhg official? Sometimes public comment undeservedly glorifies an individual who is lkeaving the party. I would just wish the person well and proceed with business as usual. Ronald Reagan was once a Democrat.
mchilyi
Tracy
Kwa vile Zitto ni mmoja wa Wanabidii, binafsi nasubiri kauli yake japo natia shaka kwani niliwahi kumuomba atupe fununu kwa nini masula ya Richmond hayakuisha bungeni kama ilivyoahidiwa na hakujibu. Ila kwa vile hili linamhusu yeye binafsi mimi sisemi kitu mpaka nimsome yeyey mwenyewe!
Jambo moja ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wa Tanzania hasa waandishi habari wanakosea ni kudhani kuwa Zitto ndiye kila kitu kwenye Chadema, yaani kuwa akitoka yeye basi CHADEMA imefika mwisho,,,,hayo yalikuwa kwenye vinavyongozwa na MREMA kwa kuwa haviendeshi kisayansi..lakini kwa chama kama CHADEMA hata Mbowe, Dk. Slaa wala Zitto akijitoa na kujisalimisha CCM kuomba madaraka…hakika CHADEMA itapwaya kwa muda kidogo ila haiwezi kusambaratika kabisa maana wataibuka viongozi wengine jasiri walioandaliwa.
Hizi taarifa za Zitto na chadema hazima maana yoyote, hatuwezi tukakaa na kuzungumzia issue kama hizi, wakati kuna mambo muhimu ya kufanya sawa ndugu zangu.
Wanasiasa hawafai, na kuhama chama si issue kwani hata hapa duniani dini haimpeleki mtu mbinguni bali inami yake mwenyewe
Sijaelewa huu mchezo wa Chadema na Zitto. Ila Wanabidii naomba msihukumu suala hili kwa haraka, kuna kitu kinafichwa. Pia kumbukeni Zitto mwenyewe alisema kati ya wanasiasa anawaona kama role model kwake ni Raila Odinga wa Kenya. Kati ya sifa za mwanasiasa huyo wa Kenya ni kuhama vyama, lakini kwa malengo. Hapo mpooo??? Mathematics of party politics. kushinda mwenye nguvu = jiunge naye pigana kutoka ndani.
Jibu ni rahisi sana! Mbowe hawezi kuwajibu sisimizi.
Kama wanataka mambo yaishe basi wawanyime hot stories. Ushauri wangu
kwa Zitto na wenzake kwa sasa ni kuwa watakuwa na hekima isiyo kifani
kama wakiamua kukaa kimya. Kwa sababu kila neno moja watakalotoa
litazaa maneno mengine 1000 (exponential amplification of the
stories). Vinginevyo mjadala wa ufisadi umepata mbadala na mafisadi
sasa wanapumua. Wakati huo wanahesabu siku na kujipanga na EPA
nyingine kuelekea Oktoba 2010
Hatuna uhakika wa kujitoa Zitto ila inaonekana yuko over ambious na
kwa umri wake angetulia na kuijenga Chadema Uenyekiti ungekuwa wake
katika muda si mrefu ujao.
Vijana wanatuvunja moyo watu wote tunaopenda mageuzi na wakati
mwingine unapata kichefuchefu.
Nilikutana na Tambwe Hiza akiwa CUF katika vijiji vya Kusini mwa
Tanzania akiwaeleza wananchi kuhusu ununuzu wa rada na ndege ya Rais
akilinganisha gharama zitazotumika na umaskini wa wanavijiji wale;leo
yuko kwingine na anaponda alikotoka na kusifia alipo.Naamini dhamira
zitawasuta wengi na hawatakuwa na amani ya moyoni kwa maisha yao
yaliyobaki.
Mh. Zitto Kabwe
Wanabidii hatuna papara bali ni jakamoyo tu kwa haya yanayonong’wa. Hebu jitokeze useme , weka taarifa sahihi kwani suala hili linakuhusu wewe binafsi. Wenge wetu tunasita kusema lolote bila kukusikia wewe kwanza. Tumia fursa hii utuambie. Vuta ujasiri useme hata kama kwa kufanya hivyo unaweza usiwapendeze miongoni mwetu.
Ikiwa hutasema lolote hapa kwenye jukwaa la wanabidii mimi sitafungua kinywa changu kusema juu yako kwani ninaweza kukosea katika kufanya hivyo.
Moderator Mh atusaidie katika hili tusihukumu mapema.
Nachangia
Mh Zitto,
Kama hayo yanayosemwa ni kweli kwa msingi kwamba lisemwalo lipo na kama halipo halijaja, nitasikitika kwamba itakuwa pigo kubwa kwa upinzani Tanzania. Mimi kwa asilimia fulani sipuuzie yanayosemwa hapa. Nilisikia kuhusu wewe kuwa unataka kugombea uenyekiti CHADEMA kabla na ikwa hivyo. Nikasikia tena kuhusu akina David na juju wakati bado mambo yako jikoni ikawa hovyo. Kuna na mifano mingine mingi ya mambo kama hayo ya watu kuvumisha ambayo yamekuja kuwa hivyo. Sisemi kwa CHADEMA tu ila kwa ujumla nimekuwa nafuatilia mambo ya home kwa njia hiyo maana niko nje kwa muda sasa na nitakuwepo huku kwa muda mrefu kiasi ijapokuwa kuna wakati nitakuja home kwa miezi kadhaa.
Sasa narudi kwenye hoja yangu ya msingi. Kuingia na kuondoka ni suala la haki ya mtu na wakati. Mimi naamini kuwa kuna wakati wa kuingia na wakati wa kutoka pia. Kuna wakati wa amani na wakati wa vita kama dini inavyotufundisha. Kuna wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokukumbatia. Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia. Jamani watu wa plagiarism hayo ni maneno ya Mfalme Sulemani ingawa nimeongezea. Kwa msingi huo jambo lolote linaweza kuwa bila hata kutaka uthibitisho wa mtu. Ni suala la wakati hasa.
Hebu tuangalie athari chache. Mimi ni mwanasiasa na mwanaharakati wa maendeleo na mambo ya utawala bora au uongozi ukipenda. Tuache hayo. Athari ya kwanza ni kuwa wewe ni mwakilishi wa kwanza jimbo lako, pili CHADEMA na tatu wapenda haki bila kusahau kuwa unawakilisha vijana wa Tanzania katika nyanja ya siasa. Najua kuna wabunge vijana hata ndani ya chama tawala ila kila mtu na neema yake alipewa na Mungu. Uamuzi wa aina yoyote utakaofanya lazima utaathiri makundi yote hayo kwa namna moja au nyingine. Bila shaka kuna washabiki wako na mimi nikiwa mmojawapo na kuna wapinzani wako wa ndani na nje. Kwa ufupi utaathiri wengi. La pili ni kwa upande wa mazingira ya siasa Tanzania.
Kama utaamua leo kutoka chama chako ina maana na ubunge hauna au kama utabaki kuwa mwanachama wa kawaida labda. Lakini lazima tujue kila mahali lazima kuna mawazo tofauti. Wazungu wanasema ‘Not one size fits all’. Wewe ni kiongozi na una maono yako. Mwenyekiti wako ni kiongozi na anayo yake. Vile vile katibu na wengine. Sasa lazima hapo maono mengine yapewe kipaumbele kidogo kuliko mengine kutokana na nani amekalia kiti cha dereva. Na hii ni sawa kabisa kwangu maana ni suala la wakati pia. Kuna wakati wa kuwa kwenye kiti cha dereva na wakati wa kuwa abiria. Na tusipokubali hili tutakuwa siyo pragmatic.
La tatu ni tafsiri watakazotoa watu. Unaweza kusema wacha watu waseme mimi nina msimamo wangu. Ukweli ni kwamba hata mafisadi wanaosemwa kila siku huwa rohoni mwao hawapendi kusemwa ila hawana njia. Vivyo hivyo na wewe usingependa watu wakujadili na kukukosoa nk. Mojawapo watasema una uchu wa madaraka ndio maana unaondoka. Uthibitisho? Ulitaka kuwa mwenyekiti na ukakosa. Kuwa mwenyekiti inaweza kumaanisha kuwa una maono ya kuingia ikulu. Hayo yote ni sahihi na haki yako. Narudia kila jambo na wakati wake. Kumbuka mwaka 1995. Kikwete alitaka kuukwaa uraisi? Akawa na subira na leo ni raisi. Tafsiri nyingine ni kwa watasema uko opportunist. Sijui kiswahili cha opportunist (fursa?). Kuwa ukiona mambo yako hayaendi unatafuta wa kumlaumu na kuhalalisha msimamo wako. Wengi sana katika siasa za TZ wako hivyo. Maslahi binafsi. Ni kama wafanyakazi. Akiona green pastures anaishia huko bila uzalendo! Tufanye utafiti. Mifano mnaijua. Tuangalie hata ndani ya chama tawala. Kuna migogoro kibao. Wanaowania uraisi ndio usiseme!
Lingine ambalo ni muhimu ni kuwa hutatoa somo la maana kwa wengine. Utakuwa umefanya jambo la kawaida tu. Fulani katoka chama hiki kaingia tawala au kingine cha upinzani! Kitu gani kipya? Wengi walishafanya hivyo mbele yako. Ni kweli hakuna jipya chini ya jua. Ila ni heri ukapata uzoevu wa mambo na ukayabadilisha taratibu ili hatimaye watu wakuheshimu!
Mimi sitaki kuingila uhuru wa mtu binafsi maana sijui kiatu chake kinabana kiasi gani. Ila pamoja na hayo wahenga wanasema mvumilivu hulambivu (mara zote) ingawaje wenye pupa husema kinyume chake (chelewa …?). Whatever, the case. Make a right decision. This requires enough time, research and multitude of counsels. Kwa sasa CHADEMA ndio chama kinachokubalika zaidi ya vyama vingine vyote vya upinzani. Vingine vimeshakuwa kama timu ya zamani ya Dar iitwayo COSMO. Vingine viko daraja la pili na vyama vngine daraja la 3 nagzi ya wilaya!
Nimalizie kwa kusema kwa msemo: ‘Mkataa pema…..?
Ndugu Wanabidii,
Tokea huyu kijana apewe kuwa kwenye kamati ya madini alishaonyesha dalili kuwa anapenda madaraka. Mtu anayependa maaraka lakini hana subira huwaga hafai. Mimi nadhani Zitto hata akirudi CCM hana faida yoyote wala sio hakuna hasara yoyote kwa vyama vya upinzani. Zitto ni sawa na mtanzania mwingine yeyote tu. Kwanza ameanza kupoteza umaarufu wake kutokana na tabisa zake zisizo na subira.
alivuma Mh Lamwai akiwa upinzani lakini akalewa madaraka na sifa za watanzania kwa sababu walimuona kama muokozi wao lakini akawasaliti sasa yuko wapi? hakuna hata anayemzungumzia! kama ni hivyo ndivyo inavyotaka kuwa kwa zitto namsikitikia sana, zitto asisahau umaarufu wake umetokana na sifa aliyopewa na watanzania wapenda mageuzi kama amelewa sifa na kujaa dharau mungu ni huyu huyu anayetoa na anayetwaa, tunasubili kupata habari zake baada ya kutoka chadema!!
Kama Zitto angekuwa Yesu au Mtume Muhammad, nawahakikishieni nisingekuwa na dini.
Zitto ni miongoni mwa Wahuni wachache waliopo pale Makao Makuu ya Chadema pamoja na kina Mtemelwa na Danda.
Ii mjue kuwa Zitto hana ADABU rejeeni mahali pooooooote alikowahi kupita halafu muone kama kuna mahali aliwahi kuishi na utawala wake wakaelewana miaka yote. Zitto kwake yeye kufukuzwa au kukimbia ni sehemu ya maisha yake.
Na ili kuthibitisha kuwa Zitto ni Mhuni tu ndani ya CHADEMA alianza kucheza na Media (tena Mwananchi) mara tu baada ya Slaa kuutangazia ummma kuwa Kafulia katimuliwa!
Unaweza kuaona adabu ya Naibu katibu mkuu…. badala ya yeye kutumia channel ile ile aliyotumia Katibu wake yeye anaanza kuropoka kwenye media.
Kina Slaa wamemheshimu tu labda kwa vile hawakuwa na uthibitisho kama yale mameno yalikuwa yake kweli au uongo…
Huyu Zitto asionekane yeye ndo CHADEMA.
SLAA, MTIMUE NA HUYU
Ndugu Angalieni Hotuba hii ya Mh Zitto Aliyowahi kuitoa Busanda Ukisoma hii hotuba kwa makini , na kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyoendelea nchini kwa sasa pengine unaweza kupata kidogo cha kustajabisha
Wakati kwa kipindi cha miaka 10, tangu mwaka 1997 hadi mwaka 2006, Bunge la Tanzania halikuwa limepata hoja binafsi kutoka kwa mbunge yeyote, Hoja binafsi ya kwanza ilitolewa na mimi Bungeni, Hoja ya Buzwagi kupinga ufisadi katika mikataba ya madini ambapo baada ya kuwashinda kwa hoja, bunge la CCM mafisadi waliamua kunisimamisha kazi yangu ya uwakilishi. Na hoja binafsi ya pili ni hoja ya ufisadi wa benki kuu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Slaa, ambayo ilikataliwa na tukaamua kuipeleka kwa Umma septemba 15, 2007 , na mpaka leo bado inaisulubu serikali ya CCM.
Tangu sekeske la Buzwagi, Agosti 14, 2007, Hali ya taifa ni tete
haijawahi kutokea tangu uhuru, na itaendelea kuwa tete mpaka hapo watanzania watakapofaidika na rasilimali za nchi yao. Na Tanzania haitafikia hali hiyo chini ya utawala wa CCM. Njia pekee ni kuondoa utawala huu uliojaa wezi, wasio na uchungu na maisha yaw ewe masikini wa Busanda.
Asiwadanganye mtu kwamba ndani ya CCM kuna kiongozi mwenye ujasiri wa kupambana na ufisadi. Mana wameanza kujitokeza baadhi ya wabunge wa CCM eti wakijifanya na wao wana uchungu na nchi hii. Eti na wao wanapambana na ufisadi. Waulizeni walikuwa wapi miaka yote hii nchi ikiuazwa? Leo baada ya CHADEMA kuhamasisha Umma kwa kupinga ufisadi, nao kwa aibu ya kuogopa kuzomewa ndio wanachukua ajenda za CHADEMA ili nao wasionekane mafisadi. Mimi nawaambia, hakuna kiongozi safi ndani ya CCM. Wabunge wote wa CCM walishinda uchaguzi Mkuu kwa takrima.
Vita dhidi ya ufisadi ni via takatifu. Haiwezi kufanywa kwa unafiki.
Wala kwa hawa ninaowaita walokole wa vita dhidi ya ufisadi..
Nimeambiwa watakuja hapa akina Olesendeka, akina Dk Mwakyembe na wenzao. Mimi nawaambia wabunge wote wa CCM walipewa shilingi milioni5 ambazo ni sehemu ya fedha za ufisadi zilizochotwa benki kuu kupitia kampuni ya kifisadi ya Kagoda. Waulizeni wakija. Mana wakati walitumia fedha za ufisadi wa Kagoda, leo wanajifanya wanapinga ufisadi. Wapi na Wapi jamani?
Mimi nawaambia kutoka uvungu wa moyo wangu kwamba, wabunge wa CHADEMA hata tufanye kazi namna gain Dodoma, kama hamna ‘mbwa’ mkali Geita, Mwanza, mtaendelea kuibiwa tu!. Tunahitaji mbwa mkali ambaye akiona ufisadi kwenye Halmashauri, RCC na Serikali kuu aje kuwaambia.
Tunahitaji mtu mwenye rekodi na tusiye na mashaka kuhusu dhamira yake ya kututumikia. Na katika wagombea hawa, hakuna Mwingine isipokuwa Magessa.
Hakuna mtu yeyote wa CCM ambaye akiwa mbunge anaweza kupinga ufisadi wa CCM ilhali wabunge wote wa CCM ni zao la ufisadi.. Labda apinge kwa unafiki wa makundi ndani ya CCM lakini sio kwa dhamira ya mapenzi ya mtanzania kwa nchi yake. Magessa amesoma sekondari Tosa Maganga, Zitto amesoma sekondari Tosamanganga. Magessa amesoma shahada ya kwanza na kufanya harakati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zitto amesoma shahada ya kwanza na kufanya harakati Chuokikuu cha Dar es Salaam. Magessa amesoma shahada ya pili Ujerumani, Zitto Amesoma Shahada ya pili Ujerumani. Ninawaomba wananchi wa Busanda, mpeni nafasi kijana wenu Finias Maggessa. Ninaamini Magessa ni Zitto na Zitto ni Magessa.
Hii ndio hotuba iliyotolewa na Naibu Katibu MKuu wa CHADEMA, Mh Zitto Kabwe . Tarehe ya Mei 09, 2009 baada ya maandamano makubwa yaliyotanguliwa na Bango lenye ujumbe “ Karibu Zitto Kabwe, Karibu Obama wa Tanzania, Mwongoze Magessa Bungeni, huku mbele yake wakiwa vijana waliobeba jeneza lililozungushwa kitambaa cha kijani katika kata ya Katoro ambayo ndio kata yenye wapiga kura wengi takribani asilimia thelathini ya wapiga kura wote wa jimbo la Busanda.
“ Leo ni furaha isiyo kifani kwa maandamano na mahudhurio makubwa kiasi hiki. Umati huu mkubwa unanikumbusha Mkutano wangu mkubwa wa kwanza kuwahi kufanya, Mkutano wa Jangwani niliofanya viwanja vya Jangwani baada ya maandamano marefu ambapo watu takribani laki mbili waliandamana na kukusanyika viwanja vya Jangwani mwezi Agosti 2007 wakipinga uamuzi wa wabunge wa chama cha mafisadi-CCM, kunisimamisha ubunge baada ya kuwashinda kwa hoja, katika mjadala uliohusu mkataba
mbovu na wakifisadi wa Buzwagi.
Ni imani yangu mahudhurio haya tafsiri yake ni imani yenu kwa mgombea wetu Finnias Maggesa. Ni imani yangu kuwa Busanda na Katoro hamtatuangusha. Viongozi wenzangu waliotangulia kuhutubia
wamezungumzia matatizo mengi yanayolikumbuka taifa letu, atatizo
ambayo kwa miaka 48 utawala wa CCM umeshindwa kuyatatua.
Mtakumbuka matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 kwa kura halali na zisizo halali yalikipa CCM ushindi wa wabunge 274 na CHADEMA wabunge 11.Lakini kwa kipindi cha miaka mitatu, wabunge 11 wa CHADEMA tumeweza kuhakikisha masuala mengi muhimu kuhusu mwenendo wa Taifa letu yanajulikana kwa Umma. Bila CHADEMA watanzania wasingejua ufisadi wa Buzwagi, EPA wala ufisadi wa Richmond uliosababisha serikali ya awamu ya nne kuanguka. Nasema kuanguka kwasababu kikatiba waziri mkuu ndio mwenye serikali. Kwahiyo serikali hii ni ya awamu ya nne na nusu.
Wananchi wa Busanda, Ingawa tupo wabunge 11, lakini CHADEMA tupo makini kukabiliana na utawala huu mbovu chini ya uongozi mahiri wa Naibu Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr Willibrod Slaa. Hii ndio sababu kwanini tunaomba mtuongezee mpiganaji wa 12, ambaye si mwingine bali kijana wenu, msomi wetu, mwenye sababu za kutosha kwa mapambano haya, Finias Magessa.
Ndugu zangu wa Busanda, Uchaguzi huu sio uchaguzi wa Ilani za vyama.
Uchaguzi wa Ilani za vyama ulikuwa mwaka 2005, ndipo vyama viliomba kura kwa Ilani , na CCM ikapata asilimia 86 ya wabunge pamoja na Urais. Mwenendo wa serikali ya CCM wote mmeouna. Wanasikitisha na kukatisha tama wananchi. Ndio maana ninawaambia, Ilani ya CCM ni ileile, kama kwa kuwapa wabunge zaidi ya 200 pamoja na Urais wameshindwa kuwatumikia, mnadhani mkichagua mbunge huyu mmoja wa CCM atabadilisha kitu? Ataongeza nini kama wenzake zaidi ya 200 wameshindwa ? Jamani CCM hawana nyongeza ya Ilani! Ni hivi hivi! Ndio maana ninawaambia kwamba uchaguzi huu ni muhimu sana sio tu kwa nyie
wakati wa Busanda, bali watanzania kwa ujumla. Ni kipimo. Ni kura ya maoni ambayo katika nchi nzima nyie watu wa Busanda ndio mmepata fursa hii ya kujibu. Mmepata fursa ya kuwaambia watawala tarehe 24, Mei mwaka huu kama mnakubaliana na mwenendo huu wa watala au hamkubaliani.
Mnaridhika au hamridhiki.
Ukipigia kura mgombea wa CCM Mei 24, tafsiri yake ni kwamba unaridhika na mwenendo wa utawala wa CCM, na ukipigia kura CHADEMA maana yake ni kwamba ni unatuma ‘signal’ kwa watawala wetu kuwa hauridhiki na mambo yanavyokwenda katika nchi yako.
Ndugu zangu wa Busanda, labda nyie hamkumbuki CCM inatupeleka awamu mmoja hadi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa ya Hali ya Umasikini na Maendeleo nchini, Mwaka 2005, Tanzania ilikuwa na wananchi ambao ni fkara milioni 11, yaani hawa wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Yaani mapato yao ni chini ya ya shilingi 1300 kwa siku.
Rais Jakaya Kikwete alipokuwa kwenye kampeni aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Na CCM ikaahidi kwenye ilani yake kwamba itapunguza idadi ya watu hawa masikini kabisa kwa asilimia 50%. Leo mwaka 2009, mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi 2010, Taarifa ya Hali ya umasikini inaonesha kuwa idadi ya watanzania wanaoishi chini ya kipato cha dola moja(shilingi 1300) kwa siku wameongezeka badala ya kupungua, na sasa wamefikia milioni12.7. Umasikini unapungua, au unaongezeka?
Hili ndilo Busanda mnalo Mei 24. Ukipigia kura CCM maana yake
unakubaliana na mwenendo wa serikali ya CCM uliosababisha idadi ya masikini kuongezeka mwaka hadi mwaka. Leo mwaka 2009 masikini kabisa wameongezeka kufikia milioni 12.7 kutoka milioni11 mwaka 2005. Maana yake katika miaka 3 CCM imeongeza idadi ya watu masikini kabisa milioni moja na laki saba.. Kwa mwenendo huu, Je kufikia kipindi cha uchaguzi wa 2010 watanazania wangapi watadumbukia kwenye shimo hilo la masikini kabisa? Milioni3? 5?.
Hii ndio maana ya uchaguzi huu. Ni uchaguzi wenu wakazi wa Busanda.
Sisi tumekuja kuwawezesha tu. Tumekuja kuwaunga mkono mfanye maamuzi sahihi kwa niaba ya watanzania wengine ambao hawakupata fursa hii.
Mkichagua CCM mtakuwa mmewaangusha watanzania. Watanzania wana imani kubwa na nyie mliochaguliwa na Mungu kupiga kura hii ya maoni!
Hebu fikiria wewe Baba na Mama wa Busanda. Mwaka 2005, katika kila wanawake 100,000, wanawake 520 walifariki dunia kutokana na matatizo ya ujauzito, Leo mwaka 2009, wanawake 527 wanafariki kutokana na matatizo ya ujauzito, matatizo ambayo msingi wake ni huduma duni za afya. Takwimu hizi maana yake nini? Maana yake katika kila lisaa limoja la Tanzania chini ya utawala wa CCM mwanamke mmoja anafariki dunia kutokana na matatizo ya ujauzito yanayosababishwa na serikali kutojali wanawake wan chi hii, na zaidi wanawake wa vijijini kama Busanda.
Hebu fikirieni ninyi wazazi na wakazi wananchi kwa ujumla. Mwaka 2005, katika kila watoto 1000, watoto 114 walipoteza maisha kwasababu ya matatizo ya uzazi, leo mwaka 2009, watoto 112 wanafariki dunia kwa matatizo hay ohayo. Tarehe 24 Mei unapokwenda kupiga kura maana yake unakwenda kujibu swali hilo. Ukimpigia kura Magessa wa CHADEMA maana yake unapinga watoto wasio na hatia kuendelea kufriki dunia kwasababu
zinazotibika kabisa. Na ukipigia kura CCM maana yake unakubaliana na mwenendo wa vifo vya watoto wasio na hatia kama hivi.
Sisi CHADEMA tunaomba utupigie kura katika uchaguzi huu ili watawala washituke, wajirekebishe. Wajue kwamba watanzania haturidhiki na mwenendo huu wa umasikini na vifo. Wewe mwananchi ukiipigia CCM kura hawatajua kama kuna tatizo, hawatajua kama wananchi wanaumia.
Hawatajirekebisha.
Hali ya Taifa hili ni mbaya sana. Na tusipoangalia, Taifa hili
tutalipeleka shimoni kabisa. Tangu mwaka 2007, Asilimia 38% ya
watanzania wamedumaa akili kutokana na lishe duni. Maana yake nini?
Maana yake katika kila watanzania 100, watanzania 38 wamedumaa akili, hawafikiri vizuri kutokana na lishe duni. Lishe duni ni ‘indicator’ ya ufukara. Kama madiwani wa CCM ni watanzania wa kawaida, basi katika kila madiwani 10, madiwani 4 wamedumaa akili. Au katika kila wabunge 10 ( wa CCM lakini), wabunge 4 wamedumaa akili kama wanatoka familia za kawaida. Hivyo hivyo kwa mawaziri wa serikali ya CCM, kwamba inawezekana katika kila mawaziri 10, mawaziri 4 wamedumaa akili.
Pengine ndio sababu wamekuwa wanasaini mikataba mibovu ya kifisadi.
Kwahiyo tarehe 24, Mei, Ukichagua CCM, maana yake ni kwamba unaunga mkono mwenendo wa serikali ya CCM kusababisha watanzania 4, katika kila watanzania 10 wawe waendelee kudumaa akili. Na ukimpigia kura Magessa wa CHADEMA, maana yake ni kwamba, unapinga , unakasirishwa na mwenendo huu. Jamani taarifa hizi hatuzitungi sisi! Wala hatuziandai sisi. Ni taarifa za serikali. Ukisoma taarifa ya serikali ya Hali ya Umasikini na Maendeleo nchini (Pverty & Human Development 2007).
Haya ndio maswali CCM wakija muwaulize, ingawa sidhani kama watafanya mikutano ya hadhara mana nimesikia wanaogopa sana kuzomewa kwa uzembe na ufisadi wa serikali yao.
Nimesikia hapa mji mdogo wa Katoro, ambayo ni makao makuu ya jimbo hamna umeme. Hamna tofauti na Kasulu wala Kibondo mkoani Kigoma.
Madhara ya kukosa umeme sio tu kwa wenye uwezo wa kuwa na umeme kukosa umeme, hali hii inasababisha gharama za maisha kuwa juu, kwasababu gharama za uzalishaji zinakuwa juu.Tulifanya utafiti Dar es Salaam kwa vijana vinyozi. Umeme ukikatika wakawasha jenereta wanatumia shilingi 68,000. Lakini wakitumia umeme wa TANESCO wanalipia shilingi 8000 tu.
Maana yake kwa kutumia umeme wa jenereta wanapata hasara ya ziada ya shilingi elfu sitini. Hii ni tafiti ilifanywa na Kamati ya bunge.
Kwaiyo sio Katoro tu. Nchi nzima ni tatizo.
Nilazima watanzania tutafakari kama tunakokwenda ni sahihi au la! Na tufanye maamuzi. Wakati tunapata uhuru, Asilimia 15 ya watanzania walikuwa na Umeme.Leo ikiwa ni miaka 48 ya Uhuru, watanzania wanaopata huduma ya umeme hawazidi asilimia 12. Maana yake katika nchi hii yenye umri wa miaka 48 ya uhuru, katika kila nyumba 100, ni nyumba 12 tu ndizo zenye umeme, ilhali wakati wa uhuru, katika kila nyumba 100, nyumba 15 zilikuwa na umeme.
Kwahiyo ukienda kupiga kura tarehe 24, Mei, unapaswa kujiuliza kama unakubaliana au hukubaliana na mwenendo huu. Ukichagua CCM maana yake unaridhika kuona kwamba wakati miaka 48 iliyopita watanzania walikuwa na huduma ya umeme ilikuwa 15, ni sawa, na sio tatizo kwa leo Tanzania huduma ya umeme kuwa asilimia 12.Naukiipigia kura CHADEMA mana yake unatma ujumbe kwa watawala kwamba unaumizwa na hali hii. Haukubaliani na hali hii.
Njia pekee yaw ewe mkazi masikini kukataa hali hii ni kukataa kuipigia kura CCM. Ni kuipigia kura CHADEMA. Ni muhimu uone kama nafasi hii adimu kuwa muhimu sana kwako. Maana uchaguzi huu umefanyika kwasababu ya mipango ya Mungu. Na tunao amini katika Mungu, tunaamini kwamba mipango ya Mungu haina makosa. Na kila mpango una busara yake.
Msituangushe kwakupewa fursa hii kabla ya miaka5 kukamilika.
Hali ni mbaya ndugu zangu. Tanzania nzima ina majimbo 232. Lakini ni ninyi watu wa Busanda mliopewa fursa ya kuchagua tena kabla ya miaka 5. Nimesikia viongozi wa CCM wakipita na kuahidi eti CCM ikishinda uchaguzi huu italeta umeme Busanda. Waulizeni walikuwa wapi miaka 48 yote hii. Kama wameshindwa kuleta ndani ya miaka 48, watawezaje ndani ya mwaka 1?
Ndio maana sisi CHADEMA tunawaambia watanzania kwamba uchaguzi huu ni kura ya maoni , Tunaamini mtachagua CHADEMA ili kuonyesha kwamba hamkubaliani. Kuna matatizo mengi sana wilaya hii ya Geita. Kwa mujibu wa taarifa za uchumi za mwaka 2006, Geita ni miongoni mwa wilaya tatu masikini kabisa Tanzania, ikiwa pamoja na Bunda na Musoma vijijini.
Ninyi wilaya yenu ya Geita, unaozalisha takribani wakia laki tatu na
nusu kwa mwaka, ambazo ni sawa na bilioni 211 kwa bei ya sasa. Lakini utajiri huo hauna tafsiri yoyote kwa maisha yenu. Sisi kwenye Kamati ya Bomani iliteuliwa kupitia upya mikataba ya madini nchini tulipendekeza kanuni ya kukokotoa mrabaha kwanza ibadilishwe kutoka asilimia tatu hadi 5, lakini zaidi hesabu hizo zikokotolewe kutokana na gharama zote za uzalishaji, na sio mwekezaji azalishe kasha aondoe gharama zote za uzalishaji kasha ndio atupe watanzania asilimia 3 tu ya hilo salio. Kwasababu CCM haina dhamira ya kuwasaidia, bado imeendelea kupiga danadana utekelezaji wa Kamati yetu.
Baada ya vuguvugu la kupinga mikataba mibovu liliasisiwa na CHADEMA tangu sekeseke la Buzwagi, Leo Geita mnapata dola laki 2 kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita( Geita Gold Mining-GGM). Kule Tarime, Halmashauri ile chini ya Uongozi wa CHADEMA, kwa kuamini kuwa wawekezaji wanatunyonya watanzania wakawaida kwasababu ya elimu duni, CHADEMA tuliamua fedha yote ile ipelekwe kusomesha watoto bure kwa shule za sekondari. Ni kweli fedha hizi ni kiduchu sana, lakini si haba. Sio sawa na kukosa kabisa. Sasa kama Tarime fedha hizi zinasomesha watoto.
Nyie wilaya ya Geita fedha hizi zinakwenda wapi? Zinaishia kwenye
warsha, vikao na makongamano ya madiwani.
Yote haya ni matokeo ya utawala dhaifu na usiowajali wa Chama cha Mapinduzi-CCM. Kwa mfano, kama Serikali ya CCM ingekubali kuetekeleza mapendekezo ya Kamati ya Bomani, Badala ya wilaya zenye migodi kupewa dola 200,000. Kila wilaya yenye mgodi ingelipwa dola milioni2 kwa mwaka. Yani mara 10 zaidi ya sasa.
Tarehe 24 Mei, ukienda kupiga kura, ukichagua CCM, maana yake
unakubaliana na utaratibu wa sasa wa CCM kutoa dola laki mbili kwa
mwaka kwa halmashauri yako badala ya dola milioni mbili kama Kamati ya Bomani inavyotaka unufaike na madini. Kura yako ni alama! Ukienda ukampigia kura Magessa, maana yake unataka Serikali ya CCM itoe dola milioni mbili badala ya dola laki mbili kwa Halmashauri yako.
Kwaiyo unaona thamani ya kura yako ilivyo kubwa. Zaidi ya utu wako, kura yako ina thamani ya mabilioni. Lakini leo tunasikia CCM wanapita wanawahonga watu shilingi elfu mbili, tatu,nne, tano. Inajua bei za wateja wake. Ukiwa mjanja mjanja kidogo inakupa hata elfu kumi. Ukiwa hujui kitu kabisa inaweza kukupa hata shilingi mia moja. Lakini wote hawa ni wajinga, tofauti yao ni bei za ujinga wao.
Ukiuza shahada yako maana yake unahujuma maendeleo ya Taifa leko.
Unahujumu maisha ya watoto wako.Lazima mjiulieze kwanini mtu akupe pesa kukuzuia usipige kura? Watoto wenu hapa wanasoma shule za kata zisizo na walimu, vitabu, wala maabara kwasababu mnakosea kupiga kura.
Kura yako ni muhimu sana. Ukipigia kura CCM maana yake unaunga mkono ufisadi. Ukipigia kura CHADEMA maana yake umeamua kuunga mkono harakati za uzalendo. CCM haijawi kuwa na huruma baada ya Mwalimu Nyerere.
Wakati kwa kipindi cha miaka 10, tangu mwaka 1997 hadi mwaka 2006, Bunge la Tanzania halikuwa limepata hoja binafsi kutoka kwa mbunge yeyote, Hoja binafsi ya kwanza ilitolewa na mimi Bungeni, Hoja ya Buzwagi kupinga ufisadi katika mikataba ya madini ambapo baada ya kuwashinda kwa hoja, bunge la CCM mafisadi waliamua kunisimamisha kazi yangu ya uwakilishi. Na hoja binafsi ya pili ni hoja ya ufisadi wa benki kuu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Slaa, ambayo ilikataliwa na tukaamua kuipeleka kwa Umma septemba 15, 2007 , na mpaka leo bado inaisulubu serikali ya CCM.
Tangu sekeske la Buzwagi, Agosti 14, 2007, Hali ya taifa ni tete
haijawahi kutokea tangu uhuru, na itaendelea kuwa tete mpaka hapo watanzania watakapofaidika na rasilimali za nchi yao. Na Tanzania haitafikia hali hiyo chini ya utawala wa CCM. Njia pekee ni kuondoa utawala huu uliojaa wezi, wasio na uchungu na maisha yaw ewe masikini wa Busanda.
Asiwadanganye mtu kwamba ndani ya CCM kuna kiongozi mwenye ujasiri wa kupambana na ufisadi. Mana wameanza kujitokeza baadhi ya wabunge wa CCM eti wakijifanya na wao wana uchungu na nchi hii. Eti na wao wanapambana na ufisadi. Waulizeni walikuwa wapi miaka yote hii nchi ikiuazwa? Leo baada ya CHADEMA kuhamasisha Umma kwa kupinga ufisadi, nao kwa aibu ya kuogopa kuzomewa ndio wanachukua ajenda za CHADEMA ili nao wasionekane mafisadi. Mimi nawaambia, hakuna kiongozi safi ndani ya CCM. Wabunge wote wa CCM walishinda uchaguzi Mkuu kwa takrima.
Vita dhidi ya ufisadi ni via takatifu. Haiwezi kufanywa kwa unafiki.
Wala kwa hawa ninaowaita walokole wa vita dhidi ya ufisadi..
Nimeambiwa watakuja hapa akina Olesendeka, akina Dk Mwakyembe na wenzao. Mimi nawaambia wabunge wote wa CCM walipewa shilingi milioni5 ambazo ni sehemu ya fedha za ufisadi zilizochotwa benki kuu kupitia kampuni ya kifisadi ya Kagoda. Waulizeni wakija. Mana wakati walitumia fedha za ufisadi wa Kagoda, leo wanajifanya wanapinga ufisadi. Wapi na Wapi jamani?
Ndio maana nawaambia kuwa uchaguzi huu wa Busanda ni wa kihistoria.
Mnayo nafasi ya kuamua kuiangusha CCM, mnayo nafasi ya kutukataa. Sisi tupo wabunge 11. Lakini kazi tuliyoifanya kwa miaka hii mitatu tunaamini, kama mnaipenda nchi yenu mtatuongezea wabunge. Tumpate mpiganaji wa 12, Ndugu yangu Finias Magesa. Mkituchagua mtakuwa mmetupa moyo, na itatusaidia kuongeza mapamabno zaidi. Lakini mkituangusha mtakuwa mnatuvunja moyo. Ni sawa na kutuambia kuwa
mapambano yetu dhidi ya ulinzi wa rasilimali za madini na vita dhidi
ya ufisadi ni kelele tupu.
Tumekuwa tukiwaambia watanzania. Mwenyezi Mungu hakudhmilia nchi hii iwe na watu masikini kiasi hiki. Hebu angalieni, Kanda ya ziwa imejaa dhahabu, Almasi, Nickeli na Almasi. Kanda ya Magharibi imejaa Shaba, Mafuta na madini ya fedha. Kanda ya kati ya ina madini ya uranium yanayotumika kutengenezea mabomu ya nuclear, Kanda ya Pwani imejaa gesi na mafuta. Kanda ya kusini imejaa makaa yam awe. Kila kanda Mungu ameipa utajiri. Lakini masikini wamejaa juu ya ardhi tajiri. Kwanini msichukue hatua? Mimi ninawaambia. Njia pekee ya kutoka hapa tulipo kwanza ni kuikataa CCM.Ndio maana ninarudia! Uchaguzi huu ni zaidi ya uchaguzi. Ni kipimo kama mnaridhika au hamridhiki na mwenendo wa utawala wa namna hii.
Katika uchaguzi wa 2005, CCM waliwaahidi maisha bora kwa kila
mtanzania kufikia mwaka 2010. Leo ni 2009, mwaka mmoja kabla ya
uchaguzi, Wangapi maisha bora walau yamepiga hodi kwao? . Mwaka 2005 bei ya kilo ya sukari ilikuwa shilingi 600, leo bei ya sukari shilingi 1400. bei imepanda zaidi ya mara mbili, Je mapato yenu yamepanda au yameshuka? Bei ya khanga za akina mama mwaka 2005, khanga ya India ilikuwa sh 2000. Leo naambiwa hapa Busanda khanga ileile inauzwa shilingi 3500. Mfuko wa saruji mwaka 2006 uliuzwa kwa shilingi 11,000.
Leo mwaka 2009 mfuko wa saruji unauzwa shilingi 21000. Mwaka 2006 nauli kutoka kijiji chochote cha jimbo la Busanda kwenda Geita ilikuwa ni shilingi 1000 mpaka 2000 tu.
Leo mwaka 2009, nauli zimepanda hadi shilingi 3000. Lazima mjiulize
kweli mapato yenu yamepanda?. Kweli haya ndio masiha bora
mliyotarajia? Wakati bidhaa hizi zinapanda bei, mazao yenu ya kilimo
kama pamba serikali imeshindwa kuzuia yasiporomoke bei. Wakati mwaka 2006 kilo ya pamba iliuzwa kwa shilingi 400, leo mwaka 2009, kilo ya pamba inauzwa kwa shilingi 300. Na haya ndio maisha bora mliyoahidiwa na CCM. Mapato yenu yanaporomoka, uwezo wenu wa kununua unashuka, lakini bidhaa za kununua zinaachwa zipande bei.
Tarehe 24, Mei ukienda kupiga kura , ukichagua CCM maana yake
unakubaliana na gharama za maisha kupanda. Ukichagua CHADEMA na Magessa maana yake unatuma ujumbe kwa watala kwamba hakubaliani na kupanda kwa gharama za maisha.
Najua kwamba watawala hawa walioshindwa wamekuwa wakitumia nguvu za dola kukabiliana na utashi wa wananchi walioamua kufanya mabadiliko.
RPC na OCD naomba mnisikilize kwa makini. Mjue kwamba chochote
mlichovaa, kuanzia kiatu, magwanda ni kodi zetu wananchi. Na labda wananchi mkumbuke kuwa hawa polisi, wengi ni watoto wa masikini kama sisi. Ni mgawanyo wa kazi, wengine wanakuwa walimu, wengine madkari, wengine polisi, wengine wabunge. Sasa kwenda kwenu upolisi kusiwafanye mgeuke tatizo kwa wananchi badala ya kuwalinda.
Polisi mnapaswa kukumbuka kuwa ninyi ni watoto wa masikini kama sisi.
Mkimtesa kijana wa Busanda, basi ujue kwamba na wewe kwenu mdogo wako anateswa na polisi mwenzako. Ukimtesa mama wa Busanda hapa, ujue kwamba polisi mwenzako anamtesa mama yako huko kwenu. Ukimtesa mzee wa Busanda, ujue na wewe wazee wako wanateswa na polisi wenzako huko kwenu.
Polisi wanapaswa kukumbuka ni sisi wabunge tunaojadili na kupitisha
bajeti zao. Na sisi wabunge wa upinzani siku zote tumekuwa mstari wa mbele kudai maslahi bora ya polisi ili kupunguza udokozi wa polisi kwa wananchi masikini kabisa, na kuwasababishia usumbufu, na kukosa amani.
Hatutaki polisi watupendelee, wala watuonee. Wakituonea tutajibu.
Wakipendelea CCM tutakataa. Polisi wanapaswa kujua leo ni polisi,
kesho raia. Hatutaki polisi waonee raia, ingawa hatutaki raia wavunje sheria.
Jamani polisi wa Tanzania ndio polisi wanaolipwa kidogo kuliko polisi
wote katika nchi kumi na mbili za SADC. Nchi zingine kama Malawi
ambazo uchumi wake unategemea tumbaku lakini polisi wake wanalipwa vizuri kuliko polisi wetu, Nchi yenye madini, ziwa, bahari, ardhi yenye rutuba, watu wenye moyo wa kufanya kazi na kila aina ya utajiri.
Polisi wanapaswa kufikiria upya kuhusu ukandamizaji wanaoufanya dhidi yetu wapinzani maana wao ni sehemu yetu. Wote tumepigika tu! Polisi ndio wanaolinda benki kuu, lakini wakati mafisadi yanaingia benki kuu, polisi wetu wanapiga ‘saluti’, mafisadi yanaingia yanachota mabilioni ya fedha, yanatoka. Polisi wanabaki ni wakukamata vibaka wanaoiba masufuria, mbuzi, kuku, na vitu vidogo vidogo. Mapapa na manyangumi yanayohujumu uchumi wetu hayaguswi.
Mimi Zitto Kabwe nawambia, sitaki kusikia mtanzania yeyote wa Busanda ananyanyaswa na polisi eti kwa sababu ya chama chake. Nikipata polisi mmoja anayenyanyasa raia kwa sababu tu ya chama chake, nitamfanyia kazi kama nilivyomfanyia Nazir Karamagi. Na nilipokuwa Tarime kwenye uchaguzi mdogo niliwaambia polisi kauli kali kwasababu ya ujinga na upumbavu wa baadhi ya polisi. Sitarajii yaliyofanywa na polisi Tarime yatajirudia Busanda. Yeyote atakaye nyanyaswa na polisi hapa atoe taarifa kwa viongozi wa CHADEMA. Ila msivunje sheria.Hatutamtetea yeyote atakaye vunja sheria. Tunataka uchaguzi wa amani, tumapate Magessa tujenge taifa hili, Kazi ambayo CCM imethibitisha kwa vitendo kuwa wameshindwa.
Tarehe 24, Mei mchague Magessa akutetee wewe mkazi wa Katoro, awatetee wakazi wa jimbo la Busanda. Awatetee wakazi wa mkoa wa Mwanza.
Awatetee watanzania. Mkoa wa Mwanza una majimbo 11, yote mkaipa CCM.
Kuna Kikao cha Kamati ya mashauriano ya mkoa, RCC, Nani atawatetea kwenye RCC ilhali mmejaza wabunge wa CCM humo?
Mimi nawaambia kutoka uvungu wa moyo wangu kwamba, wabunge wa CHADEMA hata tufanye kazi namna gain Dodoma, kama hamna ‘mbwa’ mkali Geita, Mwanza, mtaendelea kuibiwa tu!. Tunahitaji mbwa mkali ambaye akiona ufisadi kwenye Halmashauri, RCC na Serikali kuu aje kuwaambia.
Tunahitaji mtu mwenye rekodi na tusiye na mashaka kuhusu dhamira yake ya kututumikia. Na katika wagombea hawa, hakuna Mwingine isipokuwa Magessa.
Hakuna mtu yeyote wa CCM ambaye akiwa mbunge anaweza kupinga ufisadi wa CCM ilhali wabunge wote wa CCM ni zao la ufisadi.. Labda apinge kwa unafiki wa makundi ndani ya CCM lakini sio kwa dhamira ya mapenzi ya mtanzania kwa nchi yake. Magessa amesoma sekondari Tosa Maganga, Zitto amesoma sekondari Tosamanganga. Magessa amesoma shahada ya kwanza na
kufanya harakati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zitto amesoma shahada ya kwanza na kufanya harakati Chuokikuu cha Dar es Salaam. Magessa amesoma shahada ya pili Ujerumani, Zitto Amesoma Shahada ya pili Ujerumani. Ninawaomba wananchi wa Busanda, mpeni nafasi kijana wenu Finias Maggessa. Ninaamini Magessa ni Zitto na Zitto ni Magessa.
ulichokisema ni kweli kwa asilimia 100%
naomba tuungane kuwaelimisha wananchi wa Tanzania lakini tukumbuke kuwa wanaoweza kutumia internet in wachache tubuni mbinu nyingine ya kuwafikishia habari hizi.
wako Kadelya Shija Madinda