Waheshimiwa wanabidii
Tanzania tumekwisha. Nimesoma jambo ambalo haliingiii akilini mwangu katika gazeti la Mwananchi la Jumapili tar 23 Sept. lenye kichwa cha habari “MADIWANI WABAINI UFISADI UNUNUZI WA GARI LA ZIMAMOTO”
Gari lenyewe limenunuliwa kwa Tsh Mil 373, matengenezo ya gari hilo kabla ya kutumika ni Tsh Mil 400. Na bado gari hilli haliwezi fanya kazi maana bado ni bovu. Halijaweza tembea hata km 1. Ina maana hapo kuna gharama nyingi hewa ufisadi katika zoezi zima la ununuzi wa gari hilo. Ni vema kutokuwa na gari kuliko kudhani manispaa ina gari kumbe ni sawa na Box fulani tu. Napongeza Madiwani kukataa gharama hizo na kudai fedha zirudishwe. Mwisho tume imeundwa kuchungaza jambo hilo. Kuna sababu gani wakati hata mjinga anaowazi kuna UFISADI?
Suali la kujiuliza hapa ni kwamba iwapo kweli Tanzania tutakosa uaminifu kiasi hiki maisha bora yatakuwepo kweli. Kodi za wananchi kutumika ili kunufaisha wachache kiasi hiki!
Ninaonavyo mimi watumishi wote wa umma sasa wamegubigwa na ufisadi. Jamani mwananchi wa kawaida Tanzania ataishije kweli katika mmomonyoko huu wa nidhamu katika utendaji wa Serikali yetu? Majuzi madai ya waalimu kumegundulika pia watumishi hawa pia waliongeza dau ila wakagawane mbele. Ununuzi wa wa Zabuni mballi mbali za serikali nadhani ufedhuli huu upo. TUTAFIKA KWELI KATIKA HALI HII?
Ni vema tu kusema Mungu atusaidie. Sijui niseme nini zaidi!
silver
– – –
From: Sylvanus Kessy
Date: 2009/8/23
Subject:UFISADI ARUSHA