From: Admin Wanabidii
Date: 2009/8/23
Subject: Re: WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI-CC
Kadi ya CCM ni mali ya wapiganaji, mali ya Wakulima na Wafanyakazi na sii vinginevyo kwani Ilani na katiba ya chama inajieleza wazi nini ibada za chama chenu CCM..hakuna nafasi kabisa ya kundi la Pili hao wanaodai mrudishe kadi za chama.
Hakika huu ni wakati wenu Wapigaji kuhakikisha hao Mafisadi wanarudisha kadi wao na mkishindwa kufanya hilo within the next 3 Month, basi nyie nyote matapeli. yaani chama na wanachama wake ni frame tupu, bango la display njia panda.. kufurahisha macho ya wananchi.
Na hakika mwaka 2010 mtakuwa watumwa wa chama chenu wenyewe..kwa mtumwa wa kujitakia, msije huko wala sikukaribishi nyumbani kwangu!
Kifupi mkuu wangu yaani uko tayari kunyang’anywa kiunga chako!.. upo tayari kurudisha hati ya kumiliki ardhi wakati unafahamu vizuri urithi huo wazazi wako walivyoutafuta kwa taabu, leo vikaragozi visivyojaa mkononi wakuondoe wewe ktk ardhi yako mwenyewe. Comeon bro, U must be kidding me!
Nooo!.. mkuu wangu hata kama ikibidi mmalizane, CCM ife kabisaaa kabla ya Uchaguzi basi na iwe hivyo kwa sababu kama mtashindwa kujikinga na watu hawa wawili mkakimbilia vyama vya Upinzani, sijui kama wananchi watawakubali. Kwani siku zote adui mkubwa wa Mpiganaji ni POLICY,
itikadi iliyopo dhidi yake na wananchi wake na sio kupambana na
kuogopa kichwa cha mtu.,Hii ndio kwanza naiona yaani mtu unaogopa
mkono wa binadamu mwingine badala ya kuogopa kichwa..
Mkiwapisha chama basi mmeshindwa na hatuwezi kuwaachia dhamana ya National security watu kama hawa.
On Aug 22, 2:49 pm, sued Sued wrote:
Sasa kama hiyo ndiyo orodha ya wajumbe na viongozi wake wa CC na NEC, Watanzania wenzangu tusitarajie nusura ya aina yoyote, kwani hii line up ya hawa watu wa jembe na nyundo ni kuua na kufukia tu.
Na si kwamba wanachokifanya hawakielewi la hasha! Tena ukifuatilia vizuri hao ndio waumini wazuri kwa pande zote za dini wanazoamini, lakini ukweli utabaki pale pale ya kwamba matendo yako ndio nusura pekee, hata ukeshe miaka hamsini kanisani au msikitini haijalishi kama hutobadilika kimatendo.
Viongozi wa Chama tawala badilikeni sasa, wananchi tumekosa imani nanyi hadi chama.
— On Sat, 8/22/09, wambura kitigwa wrote:
From: wambura kitigwa
Subject: Re: WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI-CC
Date: Saturday, August 22, 2009, 8:51 AM
kwa wanahabari wote wenye magari na wanaotarajia kuwa na magari tafadhari hii ni lazima kusoma kwa usalama wa magari na maisha yenu na wale muwapendao.
tafadhari angalia na uwajulishe wengine ili kuzuia ajali zisizo za lazima.
2009/8/21 alade maluli
tatizo ninaloliona mimi hapo ni mfumo,
kwa mfano mtu huyo mmoja ni mjumbe wa kamati kuu,halmashauri kuu,mkutano mkuu,ni mbunge,ni waziri.
yaani anashiriki kutunga sera na kuipitisha[kamati kuu] anaitetea na inapitishwa na kikao kinachofuata[halmashauri kuu] anashiriki pia kuipitisha katika mkutano mkuu,
anainadi katika mikutano ya kampeni[akiwa mgombea-labda wa ubunge] anashinda ubunge anatakiwa akaisimamie serikali katika utekelezaji wa ile sera,
anateuliwa kuwa waziri kwahiyo anatekeleza pia hiyo sera, kwahiyo katunga sera,anaitekeleza,afu anatakiwa pia asimamie utekelezaji wake,
tatizo hatuna mgawanyo wa madaraka ya kisiasa,
ingetosha mtu kuwa mjumbe wa kamati kuu afu labda halmashauri kuu iwe na wajumbe wengine kabisa ambao wanapokea mapendekezo kutoka kamati kuu,afu na wao wayapeleke mkutano mkuu ambako pia wanakuwa sio wajumbe,pia wabunge wasiwe mawaziri ili kuacha bunge na wabunge wake wote wawe wasimamizi wa serikali na watunga sheria tu. lakini kwa staili tuliyonayo sasa ni ndoto watu hawa kutupeleka kwenye maendeleo,kwakuwa mtu huyu mmoja anakofia kadhaa ambazo akisimama kidete kwenye moja wezake wanamwita na kumbana kwenye kofia nyingine aliyonayo.
ni hayo tu wadau.
2009/8/21 Furahini Kitamana
Mungu awasamehe hawajui watendalo.
Wamefanya chama kama cha nyumbani kwao. ndani ya ccm kuna undugunization.
Wanazidi kupaka nchi matope.
Tuwaombee wajirekebishe Mungu awape ufahamu wajitambue na watambue wajibu wao kwa wananchi na siyo kuweka maslahi yao mbele na kufunika maovu wawe wazi kama baadhi ya viongozi wanavyotaka kuwa wazi nao wanawakemea.
— On Thu, 8/20/09, George William wrote:
From: George William
Subject: Re: WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI-CC
Date: Thursday, August 20, 2009, 6:59 AM
Dauda
Umefanya vema wakati mwingine ukimwomba Mungu juu ya nchi yetu taja majina haya ili Mungu aweze kusikia kilio chetu, kwa vile hawa ni viumbe wa Mungu basi si vibaya akiwaondoa wabaya wote waliomo kwenye orodha hii. Hatutasikitika hata kama wote Mungu atawaondoa kwani amewapa akili na maarifa ya kutumikia umma na wao wanafikiri NCHI ni yao na UMMA ni wao, sisi wengine wote ni wajakazi wao.
—– Original Message —-
From: “Dauda, Ibrahim (Bulyanhulu)”
Sent: Thursday, August 20, 2009 12:21:24 PM
Subject: WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI-CC
Ifuatayo ni horodha ya wajumbe wa CC ya CCM, hao ndio wenye dira ya mustakabali wa nchi yetu. Ni vizuri tukawafahamu kuliko kuwa na hisia.
WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI: (CC)
1. Ndugu Kakaya Mrisho Kikwete – Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa – Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume – Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba – Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika – Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz – Naibu Katibu Mkuu
(Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein – Mjumbe
8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa – Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha – Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi – Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa – Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa – Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour – Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela – Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati – Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala – Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe – Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh – Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta – Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho – Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah – Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz – Mjumbe
23.Dr. Mohamed Gharib Bilal – Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana – Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge – Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari – Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan – Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib – Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri – Mjumbe
30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda – Mjumbe
31 . Ndugu Abdurahman Kinana – Mjumbe
32 . Ndugu Anne Semamba Makinda – Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo – Mjumbe
34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji – Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee – Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi – Mjumbe
37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed – Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf – Mjumbe