Kwa Matishio Haya Kampuni za Antivirus Zishirikiane

Unakumbuka wakati ulikuwa unahitaji antivirus kwa ajili ya kutafuta virus ndani ya komputa ikishawapata itawaondoa kwa kuwafuta na pengine kufuta files ambazo zimeathirika na virus hao ? huo ulikuwa ni wakati wa kale kidogo kwa sasa mambo ni tofauti .

Kwa miaka 20 iliyopita watu wengi zaidi wamepata nafasi ya kutumia vifaa vya mawasiliano kama komputa na simu na aina zingine za mawasiliano hii ikalazimisha kampuni nyingi za ulinzi wa mitandao kuja na bidhaa za kupambana na uhalifu wa mitandao ndio hapo tukaanza kusikia Internet Security

Sasa kuna matishio kama spyware ambazo ni programu zinazoingia kwenye komputa kwa ajili ya kutafuta taarifa na kumtumia Yule anayehitaji au kulazimisha komputa yako na programu zake zifuate kile ambacho programu hiyo inataka kama kukupeleka kwenye tovuti fulani kwa lazima , wakati huo kupambana na spyware ulihitaji antispyware ambapo antispyware bora uliyokwepo mpaka sasa hivi ni adaware

Kuna keylogger ambazo ni programu zinazoweza kuhifadhi yale yote unayofanya kutumia keyboard ya komputa yako , kuna nyingine zinauwezo wa kuhifadhi jinsi unavyozungusha mouse ya kompyuta husika na vile unavyobonyeza au unavyofanya mabadiliko Fulani kwenye komputa hizo zamani kidogo vilikuwa ni vifaa vinavyofungwa kwenye komputa sasa imekuja kwenye programu .

Hata firewalls ambazo ni ukuta kati ya komputa na mitandao mengine duniani , firewalls zimekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya watu haswa wale wasiojua wanafanya nini kwa kulazimika kuruhusu vitu wasivyovijua au kutokuwa na taarifa nazo za kutosha .

Pamoja na hayo yote kuna Malware ambayo ni aina ya programu inayotengenezwa kwa ajili ya kuharibu utaratibu wa ufanyaji kazi wa komputa bila ya mtumiaji wa kompuya hiyo kujua tofauti na virus ambapo inaweza kuishi ndani ya komputa bila kuharibu kitu malware inauwezo wa kufanya uharibifu .

Ukaja wakati ambapo kampuni zinazotengeneza antivirus zikalazimika kubadilika kutoka kwenye programu inayofanya kazi moja peke yake yaani kupambana na virus tu , ikabidi sasa antivirus hizo kuunganisha programu zingine ambazo zingeweza kupambana na matishio mengine yanayoendelea haswa kwenye mitandao kwa njia ya mtandao .

Hapo ndipo tulipokuja kuona viongezeo mbalimbali kwenye programu nyingi za antivirus mfano kwenye mcafee kukawa na kiongezeo cha Advisor , Avg kuna Link Scanner , Symantec pamoja na Norton kuna viongezeo vipya kwa ajili ya matishio mengine ya usalama wa komputa na watumiaji wake kwa ujumla .

Pamoja na viongezeo vyote hivyo hali imezidi kuwa tete mpaka sasa hivi kwa sababu aina ya mashambulizi kwenye komputa yanabadilika kila siku na aina ya tekinologia za mashambulizi hayo zinabadilika mara kwa mara kampuni nyingi za kutengeneza antivirus zimeshindwa kwa kiasi kikubwa kuendana na mabadiliko haya kwa kiasi Fulani .

Nasema hivyo kwa sababu zile kampuni zilizokuwa zinashugulika na bidhaa ya aina moja kama LavaSoft iliyokuwa imewekeza sana kwenye Antispyware sasa imekuja na bidhaa mpya yenye uwezo wa kupambana na spyware pamoja na Antivirus kwa pamoja hii inaonyesha kwamba mtu anaweza kupenda zaidi Bidhaa za aina hii kuliko antivirus kama ilivyo zamani .

Kampuni kama ZoneAlarm ambayo ilikuwa imejikita sana katika kutengeneza programu za firewall sasa imeingiza firewall yenye antivirus maana yake ukiwa na zone alarm huhitaji tena antivirus labda kama hiyo antivirus haitoingiliana na ZoneAlarm katika utendaji wake wa kazi .

Kwahiyo tumekuja kuona sasa kwa kipindi cha sasa inabidi kampuni zinazohusika na utengenezaji wa programu hizi kushirikiana kwa kiasi kikubwa haswa kwenye database zao zinazohifadhi updates za programu zao kadhaa ili kuepuka hali ilivyosasa hivi .

Mfano unaweza kusoma toleo jipya la Virus Asubuhi ya leo kwenye tovuti ya AVG baada ya muda AVG wakawa na Dawa yake lakini itachukuwa muda kidogo kwa Symantec au Mcafee kuwa na dawa yake lakini hizo update zingekuwa zinaweza kutumika kwenye antivirus zote naamini tungefika mbali tishio jipya likija ni rahisi kushugulikia .

Ngoja tuone kwa kipindi cha Mwaka mmoja ujao hali inavyozidi kubadilika na matisho mapya yanavyozidi kutokea katika ulimwengu wa mitandao Mpaka sasa hivi hali imezidi kuwa ngumu kwa kampuni nyingi kutokana na jinsi wanavyotakiwa kushugulika na matishio mapya kila mara kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita .


Yona Fares Maro
I.T. Specialist and Digital Security Consultant

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *