From: Tuse David
Sent: Sunday, 18 October, 2009 10:58:54
Subject: Re: CHADEMA
Kuna baadhi ya watu ambao wanataka tuamini kuwa siku Tanzania ikichukuliwa na wapinzani basi matatizo yote ya Tanzania yatatoweka kama ukungu! Baadhi ya watu hawa, hawaishi kuonesha udhaifu wa chama tawala na serikali yake iliyoko madarakani. Ni watu hawa ambao kwao hakuna jema lolote, na hakuna kitu chochote kizuri ambacho kimewahi kufanywa na serikali iliyoko madarakani. Kwa watu hawa, ili kuweza kuona angalau kitu kizuri basi inabidi utumie darubini!!
> > > > > > wa Yanga wakihamia Simba na wa Simba wakihamia Yanga, bado shabiki
from Hildegarda Kiwasila
date Oct 18, 2009 5:33 AM
subject Re: CHADEMA Na Helikopta
Tuse mimi ni mmoja nisiyeamini kama upinzani utaleta mabadiliko. Toka tumeanza na baba wataifa alitegemea tutabadilika hadi leo bado. Tumesoma bure huko nyuma, tukapata scholarship, study tours ulaya, nchi za kiafrica-bado tupo ndio kwanza tunazama.
Mbona hizo nchi zote hizo ulizotaja ambako wapinzani wamechukua madaraka kumekuwa balaa. Chiluba hakutoka upinzani? Au nimechanganya? Hakuwa mtu wa labour movement akitaka kuboresha hasa? Imani ya wapinzani kufanya vyema sijaipata kwani unaona hapa bongoland nao wanagombana ktk vyama vyao, kufungiana milango etc.
Pili, tunasikia matumizi mabaya ya fedha wanazopewa za ruzuku, malalamiko ya udini na ukabila ndani ya vyama vyao. Vyama vingine unakuta ni cha mahala fulani tu mfano kina wafuasi zaidi Moshi au Pemba au Mwanza kilikoanzishwa kwengine hakina wafuasi wengi au hakuna kabisa. Vitashindaje kwa wingi wa kura na kutawala nchi? Una chama Pemba, ukatawale nchi nzima?
Makosa kama ya CCM yapo. Unakuwa Mbunge una jimbo hujibidiishi kuhamasisha maendeleo ukaonyesha mfano. Upo kuweka vikao na kulaani tu. Wananchi hawaoni unachofanya au si mfano mzuri katika jamii. Sasa helikopta, ni gharama kiasi gani? Kama angejenga visima vya maji, kuanzisha au kutafuta mhisani wa kiwanda kidogo au mashine mfano za kutoa beeswax katika asali na masega kwa wafuga nyuki, ambulance ya wagonjwa kwa zahanati; kununua mizinga ya nyuki kuwapa akina mama na vijana Moshi maana wana miti mingi na wanalinda uoto vizuri. Mzinga mmoja wa kisasa ni 20,000-28,000/= Mtu anajiwekea shamba au nyumbani kama ni zile nyuki zisizouma. Asali ya nyuki zisizouma lita TAS 6-8,000/= organic foods zinatakiwa sana duniani, bibi kizee asingepata fedha akamuona wa maana?
Helikopta si gharama zaidi? Unapita juu, chini watu wanatembeza mgonjwa kwa baiskeli kilomita kadhaa kumpeleka kutibiwa. Nyumba inawaka, mji mzima hauna gari ya zimamoto, watu wanaungua na kupoteza mali, wewe unaleta helikopta ya kuuza maneno ya siasa? Mtu hawi mjinga siku zote, watayapima haya yote. Sijashawishika.
Kingine unaona kama mtu anatoka CCM, anakwenda upinzani, anahamahama vyama kama akikosa cheo mfano kama yule anayehama hama dini. Leo RC, kesho msabato, anahama-AIC; -Kakobe;-Kwera;-last church of Jesus;-Holly Ghost; Mikocheni kwa mama Mbunge mwenye kanisa kubwa, mashule na Mikopo kwa waumini-hapo katua etc kote huko anatafuta Mungu au Yesu??? Hakieleweki na sina imani kama wakipata madaraka, kutakuwa na mabadiliko. Kutakuwa na magomvi ya vyeo.
Mwisho, mentality yetu waafrika ni moja, iwe Kenya, Tanzania, zambia etc. Ukabila, ubinafsi, udugu, uroho umetutawala; ufanisi mdogo kazini, kuabudu vya nje; kutokupenda kusoma na kugundua. Jioni aidha upo unauza utaranta, upo viti virefu au umelala. haupo katika maktaba hata kama ya home, unasoma, unapekua, unaunda, unajaribia unavumvua teknoligia. Twangoja tuletewe hata ferry ya Ukerewe au Kigamboni. Hatuundi!!
Ndio maana ukoloni mambo leo unarudi. wanarudi tena kuchimba madini, mafuta, kuanzisha viwanda, mashamba mpaka ya maua tunaajiriwa na kuyanunua maua daily gharama za ofisi, Kanisa, sherehe. Sio tuyatoe ktk bustani ya serikali karimjee, Magomeni-hizo zote zimekufa. Yanakuja kwa ndege kutoka Arusha agenti anayaleta. Tumeshindwa tumbaku, chai, mahindi, mashamba ya NAFCO ya majaribio ya minazi, ngano na mahindi ya kujaza maghala ya serikali-hata maua ya ofisi bajeti ya GVT? Ni sisi sisi sitegemei mabadiliko kama ndani ya ubongo na mitazamo yetu hatubadiliki. Ndio maana private sector utendaji wake ni kama public sector.
Hilda K
from “dr.augustine rukoma”
date Oct 18, 2009 6:24 AM
subject Re: CHADEMA Na Helikopta
Dada yangu maoni yako ni mazuri lakini naona unaelekea kukata tamaa. kama hali ndo hiyo unayosema toa mawazo au mapendekezo kupingapinga na kulalama si suruhisho. mimi ni mwanasayansi nimeone tatizo watanzania wengi wanang’olewa meno badala ya kuzibwa. sikupendezwa na hali hile nikaamua kufanya utafiti kuona nini sababu hasa ukizingatia meno bandia hayafanyi kazi kama meno halisi nimepata majibu sasa nakamalishi uchapishaji wa utafiti wangu na baadae kutoa elimu kwa umma. nimekwisha toa matokeo ya awali mbele ya watafiti wa kimataifa kule mombasa kenya nitafanya hivyo mwezi wa kumi na moja hapa tanzania.na wanabidii nitawapa nakala.
si nia ya kupinga mawazo yako dada lakini kama umeona tatizo fanyatafiti mapata majibu na toa mapendekezo. kutoa mifano ya akina Chiluba sio sahihi kwanini usitoe mfano wa Ghana?
from Gululi Gululi
date Oct 18, 2009 6:52 AM
subject Re: CHADEMA Na Helikopta
Hilda, nimesoma kwa umakini ujumbe wako, ukweli nimejifunza na kugundua vitu viwili muhimu. moja, ni hali ya kukata tamaa iliyopo miongoni mwa watanzania wengi kama uliyonayo wewe juu ya mabadiriko kama yataleta ufanisi ama laa. pili nimegundua kwamba, watu wengi hatuamini katika mabadiriko.
kifupi ni kwamba, watu wengi hubeza mabadiriko, lakini ni mabadiriko hayohayo ndiyo huleta maendeleo katika jamii yoyote, waingerza wanasema, something we fear, it is fear itself:’ hiyo sipendi kuamini kuwa eti hata wapinzani wakiingia madarakani hawatafanya kitu chochote, hiyo siyo kweli kwani hata chama tawala wenyewe walianza
kwa kuwa wapinzani wa ukoloni kupitia misingi ya TANU.
Ninachoweza kusema, ni mfumo wetu wa siasa hapa nchini ambao ni tatizo na kikwazo kikubwa katika maendeleo ya siasa hapa nchini. kutokana na ukweli kwamba hakuna ushirikiano kwenye mambo yanayohusu maslahi ya nchi, iwe kwa CCM au vyama vya upinzani. kwa upande wa vyama vya upinzani wao wana kitu ambacho kinaitwa ” To oppose, everything, to propose nothing untill the downfall of the government” na kwa upande wa CCM kwa upande wao wanakitu kinachoitwa, ” to reject everything, to agree nothing untill the demise of opposition party”. hiyo ndiyo tatizo katika mfumo wetu wa siasa hapa nchini.
Lakini siyo kweli , kwamba hata wapinzani wakiingia madarakani hawatafanya kitu. kwani huwezi kukosoa kitu kama ni kibaya, wakati hujakipa dhamana ya kuongoza. Mwanazuoni moja aliwahi kusema kwamba, “we are the change we wish to see”
from Hildegarda Kiwasila
date Oct 18, 2009 12:25 PM
subject Re: CHADEMA Na Helikopta
Thanks Gululi,
Hayo ni mawazo yangu tu na wasi wasi wangu. Ila angalia kitu kinachoendelea, onyesha indicator ya kule ambako kuna mbunge wa upinzani ambaye ni tajiri ana mahelikopta, viwanda ameleta mabadiliko yanayoonekana katika jimbo lake au kata yake anapoishi ikawa inawika tukaisikia kuwa ya mfano. Ninawaomba wao wafanye tathimini na watoe makala za vitabu watuonyeshe hayo na vigezo.
Kingine ni pale mimi ninapoona migogoro vyamani mwao kama CCM. pamoja na kuwa chama kipo eneo fulani tu-Pemba, Mwanza, Bukoba kwingine hakuna au finyu. pamoja na haya unakuta kama usemavyo ni kupinga kupinga, kupingua kwa mifano no-kama ule waraka unaosema-wao wamesoma sana, wana mahospitali-wewe husomi why?
Mwisho ni pale, inapofuka kutuoa mgombea-kila mmoja anataka nkugombea yeye awe Rais. hawatoi mgombea mmoja, wanaliona chaguzi zote, wanatawanya kura, CCM inachukua nafasi, wanaanza tena kubwata kupinga na bila kupingua. wengine wapo vile vile kama hivyo CCM waisemayo-wanagombea, wanaafya mbaya, wanaumwa, hawaachii wengine na wanawafungia nje? demokrasia itakuja kweli. Nyerere alisema kweli-hakuna chama tena kama CCM, wengine wote wana matatizo, ikarabatini CCM ipo hapa kudumu. na kweli itadumu. wanavyochomeana nyumba, kumwagiana kinyesi, ukabila, udini uliwazi-watu watasema., mmmmh bora jini likujualo. Tunatishwa?
Ktk Vyama vyote, si uongo nikisema hata kama si mwanachama wao-Ninaimani na Chadema tu. lakini bado ninawasiwasi mwingi. Sina haja ya kujaza karatasi. hata kama ni mchumba anayehangaika-si mpaka atoe mahari ndio uone ni kweli. Na uongo-mpaka muingie kanisani au msikitini yaani aonyeshe mfano ndio uamini.
Thank you.